“Zanzibar inathamini michango inaotolewa na taasisi za kiraia” – Mhe. Harusi Said Suleiman

0

Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imesema inathamini michango inayotolewa na taasisi za kiraia katika juhudi za kukabiliana na maradhi yanayosababishwa na virusi vya corona.

Akizungumza baada ya kupokea msaada wa vifaa kinga dhidi ya maradhi hayo vilivyotolewa na jumuiya ya waratibu na waendeshaji wa shughuli za utalii zanzibar naibu waziri wa afya harusi said suleiman amesema msaada huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kujikinga na maradhi hayo.

Aidha amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari juu ya kujikinga na maradhi hayo kwa kufuata miongozo na utaratibu uliowekwa na serikali.
Nae mwenyekiti wa jumuiya hiyo hassan ali mzee amesema msaada huo ni wa awamu ya mwanzo ambapo awamu ya pili wanatarajia kuelekeza msaada wao katika sehemu za kijamii.