Categories
E! News

‘Watatu Flavor halitovunjika kwa sababu tunaishi kwa kuheshimiana’ – Wigo Flavor

Waswahili wanasema: Kwenye wengi siku zote hapakosi kasoro. Msanii anayeunda kundi la Watatu Flavor, Wigo Flavor azungumza kuhusiana na matatizo yanayosababisha makundi mengi kutodumu kwa muda mrefu.

watatu

Akiongea na Zenji255 Wigo amesema kuwa kwa upande wamejipanga na uzuri uliokuwepo kati yao ni kujuana kwa muda mrefu kitabia pamoja na kufanya kazi pamoja.

“Kwanza, tumeekeana mipaka, yaani tunaishi kwa kuheshimiana. La pili, tunaishi katika hali ya ukweli hatufichani chochote. Makundi mengi hayadumu kwa sababu ya kufichana na hakuna kibaya kinachofanya hata ndugu wa familia kugombana. Kwetu sisi hilo tumejipanga na kama litatokea tutalimaliza bila matatizo .” Amesema mmoja ya wasanii wa kundi Wigo Flavor.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.