Categories
Music

New Music: Rico Single ft. Smile The Genius & Black Fit – Bend Over

Kutokea visiwani Zanzibar, wimbo mpya kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya Rico Single. Wimbo unaitwa “Bend Over”, akiwa amewashirikisha Smile The Genius na Black. Wimbo umetayarishwa na producer na Aloneym katika studio za Island Records.

Sikiliza wimbo huo na utoe maoni yako.

Categories
Z! Extra

Barrack Obama akosoa viongozi wenye kutoa kauli za kibaguzi na chuki

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama amewataka Wamarekani kukataa lugha za chuki na kibaguzi kutoka kwa viongozi wao.

Obama amekuwa akiongea kwa nadra tangu alipoondoka madarakani, na japo hakumtaja kiongozi yeyote kwa jina, lakini kauli yake hiyo imekuja baada ya rais Donald Trump akiwa katika harakati za kujinasua kuwa kauli zake dhidi ya wahamiaji ndizo chanzo cha kuchochea mauaji nchini humo.

Katika hotuba yake jana Jumatatu, Trump alikemea ubaguzi wa rangi. Jumla ya watu 31 wameuawa katika mashambulio ya bubduki kwenye majimbo ya Texas na Ohio mwishoni mwa wiki.

 

Akiwa madarakani, Obama alipigana pasi na mafanikio kudhibiti umiliki wa silaha za moto nchini Marekani. Aliiambia BBC mwaka 2015 kuwa, kushindwa kupitisha kwa sheria za kudhibiti silaha ndilo jambo kubwa alilofeli akiwa kama kiongozi wa nchi hiyo.

Trump kulipa kisasi kwa ”upumbavu”wa Macron Mkuu wa ujasusi Marekani ajitenga na utawala wa Trump. Obama amekuwa akikwepa kuzungumzia sera za Trump, hususani ya uhamiaji ambayo imekuwa ikipingwa na makundi tofaouti, hata hivyo, safari hii ametoa tamko.

“Inabidi kwa pamoja tukatae lugha zinazotoka kwenye kinywa cha kiongozi wetu yoyote ambaye analisha mazingira ya uoga na chuki ama anayefanya ubaguzi kuwa jambo la kawaida. Viongozi ambao wanawafanya watu ambao hawafanani nasi kuonekana kama mashetani, ama wanaodai kuwa watu wengine ikiwemo wahamiaji wanahatarisha mfumo wetu wa maisha, ama wanaodai kuwa Marekani ni ya jamii moja tu ya watu,” amesema Obama.

Categories
Music

New Music: Aley Star ft. Rico Single – Chimba

Kama bado hujaiona video ya wimbo mpya wa Aley Star unaitwa “Chimba”, kama bado bonyeza hapa kuangalia. Katika wimbo huo Aley Star akiwa amemshirikisha Rico Single. Wimbo umetayarishwa na producer Aloneym na Razakey katika studio za Island Records.

Sikiliza wimbo huo na utoe maoni yako.

 

Categories
Videos

New Video: Aley Star ft. Rico Single – Chimba

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Aley Star ameachia video ya wimbo wake mpya unaitwa “Chimba” akiwa amemshirikisha Rico Single. Video imetayarishwa na director Eddy.

Angalia video hiyo na utoe maoni yako

 

Categories
Videos

New Video: Rico Single ft. Chege – Standard

Uliupata wimbo mpya wa “Standard” kutoka kwa Rico Single? Kama bado bonyeza hapa kuupata.

Rico Single amekuletea video mpya ya wimbo huo akiwa amemshirikisha Chege. Video imetayarishwa na director Ivan.

Angalia video hiyo na utoe maoni yako.

Categories
Music

New Music: Rico Single ft. Chege – Standard

Wimbo mpya kutoka kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya visiwani Zanzibar, Rico Single. Wimbo unaitwa “Standard” akiwa amemshirikisha Chege. Wimbo umetayarishwa katika studio za Island Records na producer Aloneym.

Sikiliza wimbo huo na utoe maoni yako.

 

Categories
Videos

New Video: Rico Single – Sakata

Baada ya kuachia wimbo wa kusikiliza wa ‘Sakata’ hii hapa ni video yake. Rico Single amewaletea video ya wimbo huo ‘Sakata’. Video imetayarishwa na director Sam.

angalia hapo chini na utoe maoni yako.

 

Categories
Music

New Music: Rico Single – Sakata

Huu hapa ni fungua mwaka 2018 kutoka kwa Rico Single na wimbo wake mpya unaitwa ‘Sakata’. Wimbo umetayarishwa katika studio za Island Records chini ya producer Aloneym.

Sikiliza hapo chini na utoe maoni yako.

 

Categories
Videos

New Video: Pozza Boy ft. Linex & Rico Single – Madebeni

Pozza Boy ameachia video ya wimbo wake mpya ‘ Madebeni’ akiwa amemshirikisha Linex na Rico Single. Video imetayarishwa na Director Ivan.

Angalia video hiyo hapo chini

 

Categories
Videos

New Video: Rico Single, Baby Jay & Pozza Boy – Nakiwasha

Rico Single ameachia video mpya inaitwa “Nakiwasha” akiwa ameshirikiana na Baby Jay na Pozza Boy. Video imetayarishwa na Director Juhudi.

Angalia hapa

 

Categories
Videos

New Video: Rico Single – Halindwa

Msanii wa muziki Rico Single ameachia video ya wimbo wake mpya “Halindwa”. Video imetayarishwa na director Ivan.

Angalia hapo chini

Categories
Photos

Picha: Rico Single alivyotoa burudani Full Moon Party Wikiendi hii

Msanii wa muziki Rico Single aliweza kuzifurahisha nyoyo za wageni mbali mbali waliofika katika Full Moon Party iliyofanyika siku ya Jumamosi (Machi 11) katika ufukwe wa Kendwa Rocks iliyopo Nungwi, Zanzibar.

Katika onyesho hilo lilifunguliwa na kikundi cha ngoma za asili na kufuatiwa na Muimbaji kutoka Jamaica, Pampi Judah ambaye alitoa burudani ya raggae vizuri na baadae kufuatiwa na Rico Single aliyepanda kwenye steji na Live band.

Angalia picha za onyesho hilo lilivyokuwa

This slideshow requires JavaScript.

Categories
Photos

Picha: Rico Single, Bob Maghrib & Batimbo walivyotoa burudani kwa wageni katika Tamasha la Sauti za Busara

Ikiwa imebakia siku moja kuendea tamati, wasanii kutoka nchi za mbali mbali za Afrika walitoa burudani katika tamasha la Sauti za Busara kwa wageni mbali mbali walioshiriki katika viwanja vya Ngome Kongwe Zanzibar.

Wasanii kama Bob Maghrib (Morroco), Rico & The Band na Batimbo Percussion Magique kutoka Burundi, walitoa burudani ya kutosha na kuweza kulipamba vizuri tamasha kwa siku hiyo.

Angalia picha hapo chini (Picha zote: Othman Maulid)

This slideshow requires JavaScript.

Rico Single & The Band at Sauti za Busara

Categories
E! News

Rico Single kuachia wimbo wake mpya katika Tamasha la Sauti za Busara

Ikiwa kama ni suprise kwa mashabiki wake, Msanii wa muziki wa kizazi kipya Rico Single amesema anataka kuwapa zawadi ya wimbo wake mpya mashabiki ambao watakaohudhuria siku ya atakayofanya show yake katika tamasha la Sauti za Busara siku ya Ijumaa (Feb. 10) Ngome Kongwe.

riso single

Akiwa mmoja ya wasanii watakaoiwakilisha Zanzibar katika tamasha hilo kupitia muziki wa kizazi kipya, Rico Single amesema kuwa matayarisho yote yapo tayari na sasa anajiandaa kufanya mazoezi na bendi kwa ajili ya onyesho lake.

“Mazoezi tayari tumeshaanza na kila kitu kipo sawa, nimejiandaa vizuri. Na siku hiyo nataka niwape zawadi mashabiki wangu watakaokuwepo katika tamasha hilo wimbo wangu mpya ambao nitakuja kuuachia baada ya hapo. Wimbo umetayarishwa na Aloneym katika studio Island Records, watu wasubiri kwenye foleni” Amesema Rico.

Categories
Videos

New Video: Rico Single -Yani Raha

Msanii Rico Single ameachia video ya wimbo wake mpya unaitwa ‘Yani Raha’. Video imetayarishwana Director Ivan.

Angalia hapo chini na utoe maoni yako

Yani Raha Video Launch

Island Records Zanzibar Presents:

Uzinduzi wa video ya Rico Single ‘Yani Raha’. Wasanii watakao sindikiza Juma Town, Mubacriss na Sister Rahima na wengine kibao. Imedhaminiwa na Bee Fashion Zanzibar, Cowboys DJs Bomba FM na Island Records.

Categories
Videos

Video Teaser: Rico Single atoa kionjo kifupi cha video yake mpya ‘Yani Raha’

Msanii Rico Single ameachia kionjo kifupi cha video ya wimbo wake mpya ‘Yani Raha’ ambayo aliyofanya wiki kadhaa zilizopita.

Akiongea na Zenji255 Rico amesema maandalizi yote yameshakamilika na hatua inayofuata ni anasubiri ruhusa kwa uongozi wake kwa ajili ya kuachia video.

“Video ninayo mikononi mwangu na tumejaribu na uongozi wangu kuangalia kama kuna marekebisho yoyote yanahitajika lakini tumegundua hakuna na ninawaahidi mashabiki wangu muda wowote kuanzia sasa tunavyoongea video itakuwa kwenye mitandao.” Amesema Rico Single

Categories
E! News

Picha: Rico Single ashoot video ya wimbo wake ‘Yani Raha’

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Rico Single hivi karibuni alionekana akishoot video ya wimbo wake mpya ‘Yani Raha’ katika maeneo tofauti visiwani Zanzibar.

173a5098.jpg

Akizungumza na Zenji255 leo Rico, alisema ndani ya video hiyo director aliyehusika ni Ivan kutoka Dar.

“Tunashukuru mungu kazi imeenda poa, tumemaliza kushoot video na Ivan na baada ya kama wiki moja itatoka,” amesema. “Tumetumia gharama kubwa kwa sababu ya location tulizotumia ni mbali na mji, kumsafirisha pamoja na kumlipa fedha ya kazi director Ivan pamoja watu ambao walioshiriki kwenye video. Kwahiyo ni gharama kubwa kidogo sema siwezi itaja kwa sasa kwa sababu hivi ni vitu binafsi” Alimalizia Rico Single.

c360_2016-11-15-22-34-15-098.jpg

173a5157
DJ Zorro (Kushoto) Rico Single (katikati) Mass Carribean (Kulia)
Director Ivan akiwa location
Director Ivan akiwa location
Categories
E! News

Rico Single azungumzia maazimio yaliyotolewa katika kikao walichofanya na viongozi wa Zanzibar

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Rico Single amezungumzia kuhusiana na maazimio ya kikao walichofanya kati ya wasanii na baadhi ya viongozi wa serikali ya Zanzibar katika ukumbi wa ofisi ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo.

ricoKatika kikao hicho kilichohudhuriwa na wasanii wa tasnia mbali mbali hapa Zanzibar pamoja na viongozi kama Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mshauri wa Rais Mambo ya Habari, Mshauri wa Rais mambo ya Sanaa, Utamaduni na Michezo pamoja na Mwenyekiti akiwa na Katibu Mkuu wa Baraza la sanaa Zanzibar.

Akizungumza na Zenji255 Rico Single amesema kuwa tamati iliyomalizwa katika kikao imewapa moyo wasanii wengi waliohudhuria na kama viongozi watayashughulikia kwa moyo mmoja na kuyafanikisha basi sanaa ya Zanzibar itafika mbali.

“Kiukweli mambo mengi tumeongea na uzuri kwamba wasanii wengi walikuwa wana hamu na fursa kama hii na hata mimi nimefurahia juu ya hili kwani tulikuwa na mambo mengi yanaikabili sanaa yetu ya Zanzibar na kila tukilalamika hayafanyiwi kazi vizuri” amesema Rico Single.

Haya ni baadhi ya maazimio yaliyozungumzwa katika kikao hicho ni: –

  1. Kuanzisha jumuiya ambayo itakayokuwa ikibeba na kusajili fani za sanaa tofauti tofauti wakiwemo wasanii wa Kizazi kipya, wafinyazi, Taarab, bendi za muziki na wengineo
  2. Wasanii na viongozi kukutana tena katika vikao kila mwezi ili kujadili changamoto zinazotokea katika kila mwezi.
  3. Kuweka utaratibu wa kazi ya sanaa ikiwemo kuweka bei maalum kwa wasanii wanapoenda kufanya kazi wawekewe kiwango chao kwa mameneja wanaotaka kufanya nao kazi.