Categories
Z! Extra

Barrack Obama akosoa viongozi wenye kutoa kauli za kibaguzi na chuki

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama amewataka Wamarekani kukataa lugha za chuki na kibaguzi kutoka kwa viongozi wao.

Obama amekuwa akiongea kwa nadra tangu alipoondoka madarakani, na japo hakumtaja kiongozi yeyote kwa jina, lakini kauli yake hiyo imekuja baada ya rais Donald Trump akiwa katika harakati za kujinasua kuwa kauli zake dhidi ya wahamiaji ndizo chanzo cha kuchochea mauaji nchini humo.

Katika hotuba yake jana Jumatatu, Trump alikemea ubaguzi wa rangi. Jumla ya watu 31 wameuawa katika mashambulio ya bubduki kwenye majimbo ya Texas na Ohio mwishoni mwa wiki.

 

Akiwa madarakani, Obama alipigana pasi na mafanikio kudhibiti umiliki wa silaha za moto nchini Marekani. Aliiambia BBC mwaka 2015 kuwa, kushindwa kupitisha kwa sheria za kudhibiti silaha ndilo jambo kubwa alilofeli akiwa kama kiongozi wa nchi hiyo.

Trump kulipa kisasi kwa ”upumbavu”wa Macron Mkuu wa ujasusi Marekani ajitenga na utawala wa Trump. Obama amekuwa akikwepa kuzungumzia sera za Trump, hususani ya uhamiaji ambayo imekuwa ikipingwa na makundi tofaouti, hata hivyo, safari hii ametoa tamko.

“Inabidi kwa pamoja tukatae lugha zinazotoka kwenye kinywa cha kiongozi wetu yoyote ambaye analisha mazingira ya uoga na chuki ama anayefanya ubaguzi kuwa jambo la kawaida. Viongozi ambao wanawafanya watu ambao hawafanani nasi kuonekana kama mashetani, ama wanaodai kuwa watu wengine ikiwemo wahamiaji wanahatarisha mfumo wetu wa maisha, ama wanaodai kuwa Marekani ni ya jamii moja tu ya watu,” amesema Obama.

Categories
Videos

New Video: Ison “Zenj Boy” Mistari ft. G Nako – Mazabe

Video ya wimbo mpya kutoka “Zenj Boy” Ison Mistari unaitwa “Mazabe” akiwa amemshirikisha G.Nako. Video imetayarishwa na director Hanscana.

Angalia video hiyo na utoe maoni yako.

Categories
Videos

New Video: Wigo ft. Public & Ison Mistari – Nipe

Baada ya kuusikiliza wimbo mpya wa Wigo Fleva unaitwa “Nipe” hii hapa ni video ya wimbo huo akiwa amemshirikisha Public na Ison Mistari. Video imetayarishwa na director Japheth.

Angalia video hiyo na utoe maoni yako.

Categories
Music

New Music: Wigo ft. Public & Ison Mistari – Nipe

Wimbo mpya kutoka kwa mwanamuziki Wigo unaitwa “Nipe” akiwa amemshirikisha Public na Ison Mistari. Wimbo umetyarishwa na producer Lummie na Buju katika studio za Mandevu Records.

Sikiliza wimbo huo na utoe maoni yako.

 

Categories
Music

New Music: Zenji Boy ft Wamoto – Tunaishi Nao

Wimbo mpya kutoka kwa rapa Ison Mistari ‘Zenji Boy’ unaitwa “Tunaishi Nao” akiwa amemshirikisha Wamoto. Wimbo umetayarishwa na producer Kenny Touchez kutoka studio za Kazi Kwanza.

Sikiliza wimbo huo na utoe maoni yako.

 

Categories
Videos

New Video: Ison Mistari – Zenji Boy

Video ya wimbo mpya kutoka rapa wa muziki wa kizazi kipya Ison Mistari wimbo unaitwa “Zenji Boy”. Video imetayarishwa na studio za motion visual.

Angalia video hiyo na utoe maoni yako.

Categories
Videos

New Video: Ison Mistari – Monster

Rapa wa muziki wa kizazi kipya Ison Mistari ameachia video ya wimbo wake mpya unaitwa “Monster”. Video imetayarishwa na director Maxamilyonne.

Angalia video hiyo na utoe maoni yako

Categories
Videos

New Video: Ison Mistari – Sina Hakika na Kesho

Rapa kutoka lebo ya Stone Town Records ameachia video ya wimbo mpya inaitwa “Sina Hakika na Kesho”. Video imetayarishwa na director Dr. Tawakal.

Angalia hapo chini video hiyo na utoe maoni yako

Categories
Videos

New Video: Ison Mistari ft. Reallionare – No place like home

Umeshausikiliza wimbo mpya wa Ison Mistari? Bado Bonyeza hapa. Na kama tayari hii hapa ni video mpya ya wimbo huo. Video imetayarishwa na director Abdul Jaffery kutoka NAD.

Angalia hapo chini na utoe maoni yako.

Categories
Music

New Music: Ison Mistari ft. Reallionare – No place like home

Kutoka lebo ya Stone Town Records wimbo mpya kutoka kwa Ison Mistari akiwa amemshirikisha rapa kutoka Marekani, Reallionare Jream. Wimbo unaitwa ‘No place like home’ umetayarishwa na producer DJ Walid studio za Stone Town Records.

Sikiliza hapo chini na utoe maoni yako

 

Categories
Videos

New Video: Ison Mistari – My Talent

Kama uliwahi kuisikiliza wimbo wake, sasa hii hapa ni video mpya ya wimbo wa ‘My Talent’ kutoka kwa Ison Mistari. Video imetayarishwa na Mirjam Berger na Pius Bacher.

Angalia hapo chini na utoe maoni yako.

 

Categories
Music

New Music: Shamy Boy ft. Ison Mistari – Kanipa

Rapa kutokea lebo ya Stone Town Records, Shamy Boy ameachia wimbo wake unaitwa “Kanipa” akiwa amemshirikisha Ison Mistari. Wimbo umetayarishwa katika studio za Island Records na producer DJ Walid.

Sikiliza hapa na utoe maoni yako

 

Categories
Music

New Music: Ison Mistari – My Talent

Rapa kutokea lebo ya Stone Town Records, Ison Mistari ameachia wimbo wake mpya unaoitwa ‘My Talent’. Wimbo umetayarishwa katika studio za Stone Town Records na producer DJ Walid.

Sikiliza hapa na utoe maoni yako.

 

Categories
E! News

Hizi hapa ni sera 3 endapo Ison Mistari atapewa nafasi ya kugombania urais

Kila binadamu huwa na ndoto kubwa zinazoweza kusaidia kuleta mafanikio kwa njia moja ama nyingine ili kuweza kujikwamua na umaskini. Kwa rapa Ison Mistari amefunguka na sera 3 endapo yeye atakapo kuwa mwanasiasa na kupata nafasi ya kugombania urais atasimamia nini?

Ison

Ison Mistari amesema kwa upande wake hatotaka kabisa kujiingiza katika mambo ya siasa ila ametoa mifano endapo atapewa nafasi hiyo.

Haya hapa ni mambo 3 endapo Ison Mistari akipewa nafasi ya kugombani urais atahakikisha kuyafanya.

  1. Kuwarahisishia watu mzunguko wa pesa kuwa mwepesi

Kwa sasa kwa upande wa Zanzibar mzunguko wa pesa umekuwa mdogo na sio kama vile zamani kulivyokuwa na bandari huru. Biashara zilikuwa nyingi mpaka inafikia hatua wageni mbali mbali kutoka Comorro, Tanga, Mombasa na Dar es Salaam walikuwa wakifika Zanzibar kufanya biashara pakiwa ni kituo kikuu cha biashara maarufu kama ‘Used’.

2. Kulirudisha soko la muziki Zanzibar

Soko la muziki kwa Zanzibar kwa sasa lishaibiwa na halipo tena, wasanii tunahangaika na hatujui tutaupeleka wapi muziki wetu, zaidi ya kuishia maredioni na kuzihifadhi CD zetu majumbani. Zanzibar ilikuwa ndio sehemu ya kwanza kuanzishwa kwa muziki wa kizazi kipya, wasanii wa bongo kama Kwanza Unit walikuwa wanakuja Zanzibar kushoot na kutengeneza nyimbo zao. Mimi nilikuwa katika kundi linaitwa Wanduza Family na tulishawahi kuuza nyimbo zetu katika maduka kama vile Alakeyfak na tulifaidika kwa mauzo yale kwa kipindi kile, lakini sasa hivi hakuna pa kuuza.

3. Kuwapa fursa wawekezaji wote kuwekeza katika soka la Zanzibar

Soka la Zanzibar linazidi kwenda chini siku hadi siku, na hii yote ni baada ya kukosa wadhamini katika soka. Wawekezaji wameekewa vikwazo kwamba kampuni za pombe haziruhusiwi kudhamini soka letu lakini, Bar bado ziko wazi, Kwenye luninga matangazo ya pombe kila siku yanaonyeshwa, watoto wadogo siku hizi wanakunywa pombe tena hadharani. Inatubidi tubadilike na tuangalie wapi tunaweza kusaidia juu ya hili, hata kama sio lazima hao wadhamini wa pombe lakini kama serikali tunao uwezo wa kupata wadhamini wakubwa wa kuliendesha soka letu la Zanzibar.

Categories
E! News

Picha: Ison alivyotoa burudani katika Usiku wa Tamaduni Muzik

Show ya Tamaduni iliyofanyika Jumamosi hii katika viwanja vya Kilinge jijini Dar es salaam ilikuwa ni show ya aina yake ambapo ilishirikisha marapa mbali mbali kutoka jijini akiwemo na rapa Ison Mistari ambaye alipata mualiko kuonyesha makali yake.

Show hiyo ilikuwa maalum kwa wasanii wanaotokea katika lebo hiyo na wanaofanya muziki aina Hip Hop ambapo alionekana rapa kama One the Incredible pamoja aliambatana na timu nzima ya Stone Town records.

Angalia picha za show hiyo ilivyokuwa

Dj Walid kutoka Stone Town Records
Ison akiwa jukwaa moja na One The Incredible

Categories
Videos

New Video: Ison Mistari – Nani Nilimkosea

Msanii wa muziki, Ison Mistari ameachia video ya wimbo wake ‘Nani Nilimkosea’. Video imetayarishwa na Director Abdul Jafary (NAD Edutainment).

Categories
Photos

Picha: Siti & The Band, Ison Mistari, Kali na Asali walivyotoa burudani katika uzinduzi wa video ya ‘Nani nilimkosea’

Siku ya Jumapili (Feb .5) Ilikuwa ni usiku wa uzinduzi wa video mpya ya ‘Nani Nilimkosea’ ya rapa Ison Mistari.

Kiukweli watu wengi walifurahi Mapinduzi ya uzinduzi huo. Burudani nyingi zilifanyika, wasanii na wadau mbali mbali wa burudani walihudhuria katika uzinduzi huo. Vikundi vya burudani kama Wakushi band, Kali na Asali, Siti & The Band, Alfa na Ison Mistari walitoa burudani katika shuhuli hiyo.

Angalia picha jinsi uzinduzi huo ulivyokuwa.

This slideshow requires JavaScript.

Ison Video Release ‘Nani Nilimkosea’

Stone Town Records Presents: Ison Mistari ‘Nani Nilimkosea’ Official Video Release.

Categories
E! News

One The Incredible, Ison Mistari na Clint Fierce kuachia collabo yao Machi 3

Ikiwa imesalia siku moja kuendea uzinduzi wa video yake mpya siku ya Jumapili (Feb.5), kuna collabo ambayo Ison Mistari ameshirikishwa na rapa One the Incredible pamoja na Clint Fierce inayoitwa ‘My City’.

ison mistari

Hiyo itakuwa ni collabo ya pili kwa msanii huyo ambapo ya kwanza alifanya rapa kutoka Marekani Reallionare Jreams. Wimbo huo unatarajiwa kuachiwa Machi 3 ambao umetayarishwa katika studio za Stone Town Records na producer DJ Walid.

Categories
E! News

Sultan King, Ison Mistari kuzindua video zao wikiendi hii

Katika moja ya ahadi zilizokuwa zinasubiriwa kutimizwa kwa mashabiki wa muziki ni hizi hapa. Wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Sultan King na Ison Mistari watafanya uzinduzi wa video zao katika siku tofauti na kumbi tofauti hapa Zanzibar.

Mnamo siku ya Jumamosi (Feb. 4), Sultan King atazindua video yake mpya ‘Sitaki Lawama’ katika ukumbi wa Chukwani Mess ‘Intebe’. Ikumbukwe kuwa Sultan alitakiwa kuzindua video yake hiyo mnamo Jan. 28 lakini imeghairishwa.

Kwa upande mwingine Rapa Ison Mistari atazindua video ya wimbo wake ‘Nani nilimkosea’ siku ya Jumapili (Feb. 5) katika ukumbi wa Taperia, Posta ya Shangani. Katika uzinduzi huo wasanii mbali mbali watakuwepo kushuhudia video hiyo.