Categories
Music

New Music: Abramy the Voice – Naumia

Wimbo mpya kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya Abramy the Voice unaitwa “Naumia”. Wimbo umetayarishwa na producer Alex Chata kutoka studio za Dynamic.

Sikiliza wimbo huo na utoe maoni yako.

 

Categories
Music

New Music: Abramy The Voice x Smile TheGenius – Kunywa

Kwa muda mrefu wasanii waliokuwa wakifanya kazi kwa pamoja chini ya mwamvuli wa wavanilla kabla ya kuvunjika Abramy na Smile wasaniii hawa hawakufanya kazi ya pamoja kwa muda mrefu sasa wamekuja na wimbo mpya uitwao kunywa wimbo umetayarishwa katika kiwanda cha muziki serious music chini ya mtayarishaji Chidy Master
sikiliza kisha tupe maoni yako je unadhani kunahaja ya wavanilla kurudi

Categories
Videos

New Video: Abramy The Voice – Mwasi Kitoko

Msanii wa muziki Abramy The Voice ameachia video ya wimbo wake mpya unaitwa ‘Mwasi Kitoko’. Video imetayarishwa na Director Sam.

Angalia hapo chini na utoe maoni yako.

 

Categories
Music

Music: Smile & Abramy – Salome (Cover)

Wasani wa kizazi kipya Smile na Abramy wafanya cover ya wimbo wa Diamond Platnumz alioshirikiana na Rayvanny ‘Salome’.

Sikiliza hapa

 

Categories
E! News

‘Sihusiki katika kuvujisha wimbo wa Abramy aulizwe vizuri’ – Chilly K

Baada ya msanii Abramy kulalamika kuwa Producer wa Action Music kuvujisha wimbo wake mpya ‘Nashindwa’ ambao alitegemea kuuachia mwezi huu Novemba 20.
chilly k
Lakini katika kila malalamiko, ni vyema kusikiliza pande zote zinazohusika kwenye jambo husika ili kuupata ukweli. Action Music ndio walioutayarisha wimbo huo wamezungumza kuelezea mambo yalikuwaje.
Producer wa studio hiyo, Chilly K ameiambia Zenji255 kuwa yeye hana taarifa yoyote ya wimbo huo kuuvujisha, kwani siku iliyorekodiwa wimbo huo walikuwepo wawili tu na hakuna alieondoka na wimbo.
“Ngoma  ipo tayari na ilikuwa katika masahihisho madogo madogo ya kumaliziwa ili iende redio, lakini mimi sihusiki katika kuvujisha. Uongozi wangu hauniruhusu mimi kupeleka nyimbo za wasanii redio. Kuna watu maalum wanahusika katika upelekaji redio, Itabidi aulizwe vizuri (Abramy) kuhusiana na hili mwenyewe itakuwa anamuelewa mhusika aliyefanya hivyo” amesema Chilly K.
Categories
E! News

Abramy amlaumu Producer Chilly K kwa kuvujisha wimbo wake

Msanii wa miondoko ya Zenji Fleva Abramy the Voice, ametoa lawama zake kwa Producer wa studio ya Action Music, Chilly K baada kuvujisha wimbo wake.

abramyHii imekuja baada ya nyimbo hiyo kuachiwa bila ridhaa yake. Abramy amesema kuwa huo wimbo ameufanya muda mrefu na mategemeo yake ilikuwa auachie Novemba 20.

“Nimejisikia vibaya sana tu, nimeona kama nahangaika kufanya kazi halafu mtu kazi yangu anaichukulia masihara tu, mimi nina uhakika wa wimbo wangu umevuja na Chilly K ndie aliyevujisha na sijui lengo lake ni nini” Amesema Abramy.

Aliongeza na kusema “Kawaida producer anapotengeneza wimbo hubakia studio na mimi siwezi nikafanya wimbo halafu nikaachia kizembezembe, yeye ndie anahusika.  Ni tayari kwamba nishakula hasara juu hili na sina jinsi, kikubwa kama watu wakiichagua na kutaka ichezwe basi ni ruhsa kufanya hivyo ” alimaliza Abramy.

Categories
E! News

Hili sasa ni ‘beef’ maradufu kati ya Good Father Entertainment na Abramy

Hivi karibuni kwa hali ya kushangaza msanii Abramy alionekana amepost katika mitandao ya kijamii maneno ya ugomvi kwa uongozi wa Good Father Music.

Abramy aliandika katika ukurasa wake wa facebook kuwa “Masharti yatawashinda hawa… Licha kuwa mziki mgumu lakini sio kwa kuranda na msukule kila mahala….. “

hk_abramy

Haijajulikana chanzo ni nini mpaka msanii huyo kuamua kuandika hivyo ila Zenji255 iliongea nae na kusema kuwa “Hapana, sijamaanisha ugomvi nao ila niliongea kutokana na mambo ninayoyaona kila siku katika harakati zao. Na ndio maana nikayasema maneno yale ila sina ugomvi nao.”

Lakini kwa upande wa uongozi wa Good Father hawakuweza kuzungumzia lolote kuhusiana na hilo.

Categories
E! News

GoodFather Music huenda ikamsaini Abramy

GoodFather Music Entertainment kama inavyofahamika na wadau wengi wa burudani ni management ambayo iliasisiwa na mwanaharakati wa muziki kutoka visiwani Zanzibar anayefahamika kwa jina la Khamis HK.

hk_abraKwa kiasi kikubwa uongozi huu umefanikiwa kuwasaidia baadhi ya wasanii hapa Zanzibar na tena sio wasanii wa muziki wa kizazi kipya tu bali hata wa maigizo.

Lakini kwa siku za hivi karibuni kupitia Instagram ya uongozi huo iliandikwa taarifa ambayo inamhusisha msanii kutoka katika kiwanda cha Zenji na Bongo Flava, Abramy kuwa yupo katika mazungumzo na uongozi huo kwa ajili ya kumsimamia kazi za muziki wake. Tetesi ambayo iliasisiwa na boss wa management hiyo ya GoodFather Music, Khamis HK.

 

 

 

Categories
E! News

“Wimbo wa Hawalali umenipatia ‘Connection’ nyingi” – Abram The Voice

Na Mkali Nesta

Msanii wa mziki wa kizazi kipya Zanzibar Abramy TheVoice amesema wimbo wake wa hawalali umempatia connection nyingi za ndani na nje ya zanzibar. Akizungumza na Zenji255 abramy amesema “kwanza nashukuru sana unajua hawalali ni ngoma kubwa sana na imeniweka katika position nzuri katika mziki imenipatia  ‘connection’ nyingi sana za ndani na nje ya zanzibar” amesema abramy. Hata hivyo star huyo ameshindwa kuweka wazi siku gani video ya hawalali itakua tayari kwa upande mwengine abramy aliutaja wimbo anaoupa heshima kuliko nyimbo zote alizowahi kuimba “kiukweli wimbo ambao naupa heshima kubwa chakachua kwasababu ndio wimbo ulinitambulisha watu wakanifahamu” alimalizia Abramy.

Categories
Music

Music: Classmate ft. Abramy – Dedication

Classmate msanii anayechipukia kutoka Zanzibar, wimbo wake mpya akiwa amemshikirisha Abramy. Wimbo umetengenezwa katika studio za Mandevu chini ya maproducer wawili Lummie na Buju. Sikiliza Hapa.

http://www.audiomack.com/song/zenji255/dedication