Categories
E! News

Sauti za Busara 2020 na kampeni dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia kwenye muziki

Wasanii wengi wa kike barani Afrika na kwingineko huendelea kupambana na unyanyasaji wa kijinsia katika tasnia ambayo inaendelea kubaki chini ya mfumo dume. Waathirika wa dhulma hizi mara nyingi huogopa kuongea kwa sababu matokeo yake yanaweza kuathiri kazi au maisha yao binafsi.

Hata wale ambao wanachagua kujitokeza kwa umma, maelezo yao hayachukuliwi kwa uzito na mamlaka kwa kuchukua hatua muhimu dhidi ya dhuluma kama hiyo. Mara nyingi kwa kuwa wana nafasi finyu, waathirika huishia kuacha mahali pa kazi au tasnia kwa jumla, lakini kwa wahusika maisha yao yanaendelea kama kawaida.

Mwaka huu katika tamasha la Sauti za Busara 2020 ambalo linatarajiwa hufanyika Mji Mkongwe, Unguja mnamo Februari 13 hadi 16, waandaaji wameamua kutilia mkazo swala hili kwa kauli mbiu inayosema ‘Pandisha Sauti Yako, Sema Hapana kwa Unyanyasaji wa Kijinsia.

Akiongea leo Yusuf Mahmoud, mkurugenzi wa tamasha hilo alisema lengo kuu la kampeni hiyo ni kubadili mitizamo, kuanzisha mazungumzo, na kuhamasisha heshima kwa wanawake kwa kuongeza uhamasishaji juu ya unyanyasaji wa kijinsia.

Anasema hii ni muhimu ili kuleta mabadiliko ya tabia na kwa sababu hiyo, ujumbe unaolenga suala hilo utafikia tamasha nzima kwa ujumla.

“Wasanii wengi wa tamasha, ndani na nje ya nchi wamekubaliana kuhakikisha kuwa kampeni hii inafanikiwa kuunganisha watazamaji wa tamasha hapa Tanzania na kwingineko, “alisema Yusuf Mahmoud.

Tamasha limeaanda shughuli zinazolingana za kukuza mifano ya jinsia, kama vile mafunzo ya usimamizi wa jukwa kwa wanawake, itakaoongozwa na mtaalamu kutoka Zimbabwe, Ushirikiano wa kisanii wa Swahili Envcounters, Circus4Life na vikundi vingine vya wanawake ambavyo vitashiriki kwenye gwaride la ufunguzi.

“Jukumu letu kuu kama waandaaji wa tamasha ni kusaidia kujenga ustadi na uwezo kwa watanzania katika tasnia ya muziki. Ninazungumzia wasaani wakiwa jukwani, na pia watu wengi nyuma ya pazia: wasimamizi, wazalishaji, sauti na mafundi wa taa na kadhalika.”

Aliongeza: “Hivi sasa nchini Tanzania, wanawake wachache ndio wanaojitokeza kuingia kwenye muziki wa asili na hii ndio sababu tamasha la Sauti za Busara 2020 tumealika wasanii kama Siti & the Band (Zanzibar), Thaïs Diarra na Mamy Kanouté (kutoka Afrika Magharibi), Pigment (Reunion), Evon na Apio Moro (Uganda). Wengine ni Circus4Life kutoka Bagamoyo, na na DJs kutoka Afrika Mashariki. Wote ni wanawake wenye shauku ambao hutumia muziki kuwasiliana na kujielezea. Wakati huo huo, wakitoa burudani nzuri!”

Yusuf Mahmoud aliongeza, “tamasha lina imani wasanii hawa wanaoshiriki watatoa msukumo, kutoa matumaini na motisho kwa wanawake na wasichana wengi ambao wanaweza pia kuzingatia kazi ya muziki.”

Tamasha la Sauti za Busara, 13 – 16 Februari 2020 linadhaminiwa na Ubalozi wa Norway, Africalia, ubalozi wa Uholanzi, Bristish Council, Zanzibar Media Corporation, Zanlink, Memories of Zanzibar Ubalozi wa Ufaransa, Emerson Zanzibar, Radio ya Chuchu FM, Mozeti, Music in Afrika na zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.