Categories
Z! Extra

Meli ya Mt. Mkombozi II yawasili Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa ahadi aliyoitowa kwa wananachi wa Zanzibar kununua meli mpya ya mafuta MT MKOMBOZI II imetimia ambapo meli hiyo imewasili Zanzibar ikitokea Shanghai nchini China.

Rais Dk. Shein akiwa Ofisini kwake Ikulu mjini Zanzibar alipata fursa ya kuiona meli ya MT MKOMBOZI II ikiwasili kutoka ukingoni mwa pwani ya Zanzibar ikitokea usawa wa kisiwa ch Chumbe na kuelekea katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja ilipokwenda kutia nanga.

Akiwa katika faranda ya jengo la Ikulu mjini Zanzibar Rais Dk. Shein alionekana akiwa na furaha kubwa wakati akiiangalia meli hiyo ikiwasili ikiwa ni kutokana na ahadi aliyoitoa na azma yake juu ya ujio wa meli hiyo mpya ya mafuta.

Meli hiyo iliyotengenezwa na Kampuni ya Damen Shipyard ya nchini Uholanzi imewasili rasmi katika Bandari ya Malindi Zanzibar majira ya saa saa tano za asubuhi na kupata mapokezi ya aina yake.

Wafanyakazi wa Wizara hiyo na viongozi wao pamoja na wafanyakazi wa taasisi nyengine za Serikali na sekta binafsi waliungana pamoja na baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika eneo la Bandari ya Malindi mjini Zanzibar kwa ajili ya mapokezi ya meli yao hiyo.

Mapema Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, mawasiliano na Usafirishaji Mustafa Aboud Jumbe akitoa taarifa kwa wananchi huko ofisi kwake Kisauni, amethibitisha ujio wa meli hiyo na kueleza jinsi hatua mbali mbali zilizochukuliwa katika mchakato wa kununuliwa meli hiyo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hadi kuwasili kwake hapa nchini.

Katibu Mkuu huyo amesema kuwa meli mpya MT UKOMBOZI II, ni meli mpya ambapo majadiliano juu ya ujenzi wa meli hiyo yalianza mwaka 2017 na mkukuku wake uliwekwa rasmi mwezi Julai mwaka 2018 na hatimae meli hiyo ujenzi wake ulimalizika mwezi April mwaka huu
2019.

Jumla ya Dola za Marekani 30.4 zilitumika kutengenezea meli hiyo ambapo ujenzi wake hadi kukamilika ulichukua miezi 18 ambapo meli hiyo ya MV MAPINDUZI II ina uwezo wa kuchukua abiria 1200 pamoja na tani 200 za mizigo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.