Categories
E! News

Mwana FA na Sallam SK wathibitisha kuwa na maambukizi ya COVID19 (Corona)

Mwanamuziki wa Bongo Flava nchini Tanzania, Hamisi Mwijuma, maarufu Mwana FA ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa amegundulika kuwa ameathirika na virusi vya COVID- 19 au corona.

FA amesema alifanya vipimo hapo jana na kupatiwa majibu yake hii leo vilivyobainisha kuwa ameathirika na virusi hivyo.

Katika kipande chake cha video alichokiweka kwenye mtandao huo, Mwana FA alieleza kwenye ukurasa wake kuwa alitoka Afrika Kusini juzi na kubaini kuwa joto lake la mwili halikuwa la kawaida.

”Sababu ya kufanya hivyo nilikuwa natoka safarini Afrika Kusini, joto langu la mwili lilikuwa halieleweki, linapanda, linashuka hivyo nilivyorudi kwa sababu habari duniani inayofahamika ni hiyo nikawa nimejitenga ili kuhakikisha siwaathiri watu wengine”.

Mwanamuziki huyo amesema kwa sasa ile homa aliyokuwa akiihisi juzi kwa sasa haipo tena lakini bado amejitenga wakati afya yake ikiendelea kuimarika.

Awali mbali na mwanamuziki huyu pia menaja wa Diamond Sallam SK naye pia amethibitisha kuwa na virusi vya corona lakini mpaka sasa amesema anaendelea vizuri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.