Categories
E! News

Ison afunguka endapo Fid Q akifanya R&B na yeye anaacha muziki kabisa

Rapa Ison Mistari amesema ataacha muziki kabisa endapo rapa anaemvutia zaidi Fid Q akiacha aina ya muziki wa Hip Hop na kuhamia katika aina nyingine za muziki.

ison

Akiongea na Zenji255 Ison amesema kuwa hawezi kuamini kwa hilo kama litatokea kwa msanii mkubwa kama Fid Q kutokana na watu wengi wanamuamini juu ya muziki anaofanya.

“Kiukweli kiupande wangu likitokea kweli hilo jambo basi na mimi naacha muziki kabisa, na sio kwamba na mimi nabadili aina ya muziki wangu nifanye R&B, Hapana, ila naacha kabisa. Kwanza, Fid Q ni mkongwe na kusaliti Hip Hop sidhani kama inawezekana maana watu wanamwaamini juu ya analolifanya na ukiangalia yeye ‘role model’ kwangu itanivunja moyo ikitokea.” Amesema Ison.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.