Categories
Z! Extra

Wawili wazuiliwa na polisi kwa kuwaua watoto waliofanya ‘haja kubwa hadharani’

Roshini, 12 na Avinash 10 walishambuliwa siku ya Jumtano walipopatikana wakifanya haja kubwa karibu na barabara moja ya kijijini, walisema.

Familia ya watoto hao waliambia BBC Hindi kwamba hawana vyoo nyumbani. Mamilioni ya raia wa India hufanya haja kubwa hadharani swala ambalo huwaweka watoto na wanawake hatarini.

Dalits wapo katika mfumo wa chini wa Hindu na licha ya kuwa na sheria za kuwalinda, wanakumbwa na ubaguzi nchini India.

”Watoto hao wawili walipigwa hadi kufa na fimbo”, afisa wa polisi Rajesh Chandel aliambia mwandishi wa BBC Shuraih Niazi.

“Tumewawekea shtaka la mauaji wote wawili. wanahojiwa”.¬†Saa chache baada ya shambulio hilo siku ya Jumatano asubuhi , maafisa wa polisi waliwakamata wanaume wawili – Rameshwar Yadav na Hakim Yadav.

Roshni na Avinash walikuwa binamu , lakini Roshni alikuwa amelelewa na wazazi wa Avinash na kuishi nao. Babake Avinash, Manoj, anasema kwamba kama mfanyakazi wa kila siku , hana uwezo wa kujenga choo katika nyumba yake.

Pia anasema kwamba ameshindwa kupata ruzuku ya serikali kama mpango wa kuwajengea vyoo watu masikini. Programu ya Swachh Bharat Mission au mpango wa usafi wa India unataka kumaliza haja kubwa za hadharani na kuimarisha usafi nchini humo.

Wakati waziri Mkuu Narendra Modi alipozindua mpango huo mnamo 2014, aliapa kuifanya India kuwa eneo la kufanya haja kubwa hadharani kufikia 2 Oktoba 2019. Kijiji cha Manoj – Bhavkhedi – kimetangazwa “kuwa kijiji ambacho hakina watu wanaofanya haja kubwa hadharani , jina mbalo serikali imekuwa ikivipatia vijiji na miji ambayo imefanikiwa kuzuia haja kubwa hadhrani.

Utafiti umeonyesha kuwa huku ujenzi wa vyoo ukiongezeka kwa kasi kubwa , ukosefu wa maji, utunzaji duni na mabadiliko ya polepoole ya tabia yamekuwa kikwazo kikuu cha kumaliza tatizo hilo.

Lakini wengi wamempongeza Bwana Modi kwa kuangazia suala hilo na kuzindua mpango huo mkubwa – ambapo wakfu wa Bill na Melinda Gates ulimtuza wiki hii , akielezea ujumbe huo wa Swachh Bharat kama “mfano kwa nchi zingine ulimwenguni ambazo zinahitaji kuboresha haraka kufikia huduma za maji safi miongoni mwa watu maskini duniani.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.