Categories
Z! Extra

“Zanzibar inathamini michango inaotolewa na taasisi za kiraia” – Mhe. Harusi Said Suleiman

Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imesema inathamini michango inayotolewa na taasisi za kiraia katika juhudi za kukabiliana na maradhi yanayosababishwa na virusi vya corona.

Akizungumza baada ya kupokea msaada wa vifaa kinga dhidi ya maradhi hayo vilivyotolewa na jumuiya ya waratibu na waendeshaji wa shughuli za utalii zanzibar naibu waziri wa afya harusi said suleiman amesema msaada huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kujikinga na maradhi hayo.

Aidha amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari juu ya kujikinga na maradhi hayo kwa kufuata miongozo na utaratibu uliowekwa na serikali.
Nae mwenyekiti wa jumuiya hiyo hassan ali mzee amesema msaada huo ni wa awamu ya mwanzo ambapo awamu ya pili wanatarajia kuelekeza msaada wao katika sehemu za kijamii.

Categories
Z! Extra

Vifaa zaidi vya uchunguzi vyahitajika kuongezeka katika bandari ya Malindi kukabiliana na Corona

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema vifaa zaidi vya uchunguzi wa maradhi ya Korona vinahitajika kwa wananchi wanaoingia na kutoka katika bandari ya Malindi Zanzibar ili kukabiliana na wingi watu wanaingia katika bandari hiyo.Naibu waziri ujenzi, mawasiliano na usafirishaji, Mhe. Mohammed Ahmada Salum amesema serikali ina wajibu wa kuhakikisha wakati wowote wananchi wake wanakuwa salama hivyo ni vyema kuona huduma zote zinahitajika katika kuimarisha usalama huo.

Amesema eneo hilo linatumiwa na watu wengi hivyo ni muhimu kuimarisha mazingira ya maeneo hayo kwa kuongeza vifaa na maeneo ya kuhifdhia watu watakaobainika kuwa na dalili za maradhi hayo.

Amevitaja baadhi ya vifaa na miundombinu inayohitajika katika maeneo hayo amesema ni pamoja na mahema, vyoo, mashine za kufanyia uchunguzi na vitu vingine vinavyohitajika katika eneo hilo.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Kapten Abdallah Juma Abdallah amesema shirika hilo litasaidia ununuzi wa baadhi ya vifaa vya kuchunguzia maradhi hayo ikiwemo mashine za kupimia joto.

Categories
Z! Extra

“Watakaokiuka agizo la Serikali la kuzuia watachakulia hatua kali za kisheria” – Mhe. Khamis Juma Maalim

Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar, Mhe Khamis Juma Maalim amesema Serikali haitowafumbia macho Wananchi wanaokaidi agizo lililotolewa na Serikali la kuzuia mikusanyiko katika maeneo yao.

Akizungumza na Vijana wa Timu ya Mpira Nyarugusu amesema Serikali imepiga marufuku mikusanyiko, hivyo Vijana hao kuendela kucheza Mpira wa Miguu katika Kiwanja hicho ni kosa kisheria.
Amesema Serikali imetoa agizo hilo si kwa ajili ya kuwakomoa Wananchi bali waweze kujikinga na kupunguza janga la Corona linaloiathiri Dunia kwa sasa, hivyo si vyema kufanya Ukaidi.
Mbali na hayo amewaagiza Viongozi wa Shehia, halmashauri na Mabaraza ya Manispaa kusimamia Agizo la Serikali na kuwafikisha katika sehemu husika watakapowabaini wanakwenda kinyume na maelekezo hayo ili wachukuliwe hatua za kisheria.

Categories
Z! Extra

COVID-19: Mwanaume aliyekiuka amri ya kukaa nyumbani aliwa na mamba Rwanda

Mwanaume mmoja nchini Rwanda ambaye alikiuka amri ya kukaa nyumbani ambayo inaendelea kutekelezwa nchini Rwanda na kuamua kwenda kuvua samaki ameuawa kwa kuliwa na mamba, Meya wa wilaya ya Kamonyi kusini mwa Rwanda ameiambia BBC.

Alice Kayitesi amesema kuwa tukio hilo lilitokea siku ya Jumatano asubuhi katika mto Nyabarongo.

“Alikua amekiuka sheria ya kukaa nyumban, alikua ni miongoni mwa watu wachache hapa ambao hawaonyeshi ushirikiano katika sheria hii ya kukaa nyumbani ili kuzuwia kusambaa kwa coronavirus ,” Bi Kayitesi amesema

Serikali ya Rwanda iliweka amri ya kukaa nyumbani siku ya Jumapili kutokana na kuendelea kuongezeka kwa kasi kwa visa vya Covid-19.
Rwanda imethibitisha kuwa na visa 40, vya maambukizi , idadi hiyo ikiwa ni ya juu zaidi kuriko mataifa mengine ya Afrika Mashariki.

Kufungwa kwa shughuli za kiuchumi katika nchi hiyo kumwewaathiri watu wengi wenye kipato cha chini.

Serikali imesema kuwa itawasaidia wale wanaohangaika wakati wa hatua kali za kudhibiti maambukizi.
Wakati huo huo idadi kubwa ya polisi wamesambazwa katika maeneo mbali mbali ya Rwanda ili kuhakikisha watu wanatekeleza amri ya kukaa nyumbani, kwa ajili ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.

Wale ambao wametajwa kuwa ni wafanyakazi muhimu, kama vile madaktari na wauguzi, wafanyakazi wa maduka ya jumla na waandishi wa habari, wanaruhusiwa kutoka nyumbani.

Categories
Z! Extra

Kampuni ya Ali Baba na Serikali ya Ethiopia yatoa msaada wa vifaa vya kupambana na Corona

Waziri wa Afya wa Tanzania, Mhe. Ummy Mwalimu amethibitisha kupokea vifaa vya kitabibu kwa ajili ya kupambana na virusi vya Corona, ambavyo ni msaada kutoka kwa tajiri mkubwa nchini China Jack MA


Vifaa hivyo ni barakoa (mask) 100,000, vipimo 20,000, na mavazi ya kujilinda (protective suits) 1,000, ambavyo vimegawiwa kwa kushirikiana na Serikali ya Ethiopia kupitia kwa Waziri Mkuu Abiy Ahmed Ali.

Categories
Z! Extra

Breaking News: Waziri wa Afya Zanzibar atangaza kisa kingine cha Corona

Waziri wa afya visiwani Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohammed ametangaza kugundulika kwa mgonjwa mwingine ambaye ana virusi vya corona.

Waziri Hamad amesema kuwa mgonjwa huyo mwanamke ambaye ni raia wa Ujerumani anatajwa kuwa alikuwa ni mpenzi wa mgonjwa wa kwanza aliyegundulika wiki mbili zilizopita hapa Zanzibar. Kwa sasa mgonjwa huyo amehifadhiwa katika hospitali ya Kidimni.

Pia ameeleza kuwa visiwani Pemba yupo mshukiwa mmoja ambae alifanyiwa vipimo na kugundulika hana ugonjwa huo na sasa amehifadhiwa karantini.

Categories
Z! Extra

Rais Magufuli apima Corona Dodoma

RAIS John Magufuli leo amepima joto la mwili katika harakati za upimaji zinazoendelea nchini na duniani kote kugundua na kukabiliana na mambukizi ya homa ya virusi aina ya Corona.

Amefanya hivyo kabla ya kuingia katika ukumbi wa baraza la mawaziri kuongoza kikao cha baraza hilo hko Chamwino, Dodoma.

Kipimo hicho hutumika miongoni mwa vipimo vya awali ambavyo hutambua iwapo mtu ana dalili za virusi hivyo kabla kufanyiwa kipimo kikubwa.

Mkuu huyo wa nchi amefanya hivyo ikiwa pia ni sehemu ya kuwahamasisha wananchi kuchunguza afya zao na kuchukua tahadhari kuhusu ugonjwa huo hatari ambao umeua maelfu ya watu duniani kote.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Makamu wa Rais, Samia Hassan; Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa; mawaziri wote, manaibu mawaziri na viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Categories
Z! Extra

Jinsi wahalifu wa mtandaoni wanavyoongeza hofu katika jamii

Wataalamu wa masuala ya usalama wamesema kuwa, mlipuko wa virusi vya corona umefanya wahalifu wa mtandaoni kutumia mwanya huu kutapeli watu pia.

Wahalifu wa mtandaoni wanawalenga watu binafsi pamoja na sekta mbalimbali kama usafiri, utalii, afya, elimu, bima na shughuli nyingine.

Barua pepe za ulaghai ambazo zinaandikwa kwa lugha ya kiingereza, kifaransa, kiitaliano, kijapani na kituruki zimebanika.

BBC imefuatilia barua hizo.

Kuna barua ambazo zinaelekeza wapi watu wanaweza kupata tiba ya corona. Watafiti katika makosa ya kihalifu wamethibitisha kuwa waligundua barua pepe ambayo hawakuielewa kutoka kwa wateja mwezi Februari.

Ujumbe ukiwa umetoka kwa daktari anayedai kuwa kuna chanjo ambayo imebainika iliyotengenezwa na serikali ya China na Uingereza.

Inawataka watu kufungua nyaraka hiyo ambayo ina maelezo kuhusu chanjo.

Barua pepe zipatazo 200,000 zimetumwa kwa wakati mmoja kwa watu tofauti. Sheria ya mtandao imesaidia kiasi gani Tanzania kupambana na uhalifu?

“Tumeona mawasiliano mengi kwa siku kadhaa ambazo zinafanya kampeni kuhusu corona ambayo haieleweki, wengi wakiwa wanawaogopesha watu ili kuwashawishi wafungue nyaraka hiyo.” alisema Sherrod DeGrippo kutoka katika kampuni ambayo inafanya utafiti wa vitisho hivyo vya mtandao.

Utafiti unasema kuwa utapeli huo unafanyika kila siku.

Ukweli ni kwamba kampeni hizi za uhalifu mtandaoni zinapata mapokeo yaliyogawanyika.

Cha muhimu tu ni kwamba watu wasifungue nyaraka hizo ambazo zinazunguka mitandaoni kuwatapeli.

Categories
Z! Extra

Rais Dk. Shein asema serikali imejidhatiti kuendeleza mapinduzi ya ilimo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesema serikali imejidhatiti kuendeleza kwa vitendo Mapinduzi ya Kilimo kwa kuwapa taaluma ya kilimo bora wakulima, wafugaji na wavuvi, pamoja na kuendeleza huduma za ugani.


Dk. Shein amesema hayo katika ufunguzi wa Maonesho ya siku ya chakula Duniani, yaliofanyika katika viwanja vya Chamanangwe, Mkoa Wa Kaskazini Pemba.
Amesema Serikali inaendelea kuweka mazingira mazuri ya kibiashara ili kuwawezesha wafanyabiashara kuingiza na kuuza zana, vifaa na pembejeo za kisasa kwa wakulima kwa urahisi.
Aidha, Dk. Shein amesisitiza haja ya wakulima kulima kwa kuzingatia matumizi ya mbinu za kisasa za kilimo pamoja na kufuata maelekezo ya wataalamu.
Aidha, amewataka Wakuu wa Wilaya kote nchini kuongeza kasi ya mashirkiano na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, sambamba na kusimamaia ipasavyo maendeleo ya kilimo katika Wilaya zao.


Mapema, Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Mmanga Mjengo Mjawiri, amesema Wizara hiyo kwamashirikiano na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali imejidhatiti kuendelea kutoa elimu kwa wananchi katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi juu ya lishe bora pamoja na matumizi endelevu ya rasilimali zilizopo, sambamba na kuwataka wananchi, hususan vijana kutumia maonesho hayo kupata ujuzi.

Categories
Z! Extra

TMA imetoa tahadhari ya kuwepo vipindi vifupi vya mvua kubwa

Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania TMA imetoa tahadhari ya siku 5 ya kuwepo kwa vipindi vifupi vya mvua nyingi katika mikoa ya ukanda wa Pwani, Visiwani Zanzibar na Kusini mwa Tanzania


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa TMA imeonesha jana kwa mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Pemba, Unguja na Kaskazini mwa Morogoro kulikuwa na mvua kali.
TMA pia imetoa angalizo kwa wakazi wa mikoa ya Lindi na Mtwara kwa kusema kuwa kutakuwa na upepo na mawimbi makubwa.
Tahadhari ya uwepo wa mvua kubwa na mawimbi makubwa imetolewa hadi Jumamosi ijayo.

 

Categories
Z! Extra

“Serikali ya Zanzibar iko tayari kushirikiana na Serikali ya Ras Al Khaimah” – Rais Dk. Shein

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kushirikiana na Serikali ya Ras Al Khaimah katika kuanzisha programu ya mafunzo kwa walimu wa Zanzibar.

Rais Dk. Shein ameyasema hayo leo wakati alipokutana na ujumbe wa Taasisi ya Sera na Utafiti ya Sheikh Saud Bin Saqri Al Qasimi huko katika ukumbi wa Hoteli ya Waldorf Astoria iliyopo mjini Ras Al Khaimah.

Ujumbe huo umekuja kufuatia agizo la Mtawala wa nchi hiyo alilolitoa kwa Msaidizi wake wa masuala ya elimu siku ambayo Mtawala huyo alikutana na kufanya mazungumzo na Rais Dk. Shein katika ukumbi wa Kasri yake iliyopo Aldhait mjini Ras Al Khaimah.

Katika mazungumzo hayo, Rais Dk. Shein ameualika uongozi wa Taasisi hiyo kuja Zanzibar kwa lengo la kukutana na uongozi wa Wizara ya Elimu pamoja na uongozi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ili kuona jinsi gani wanaweza kushirikiana katika kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu wa Zanzibar.

Rais Dk. Shein ameeleza kuwa hatua hiyo itaiwezesha Wizara ya Elimu kutoa vipaumbele vya mahitaji waliyonayo ili iwe rahisi kutekeleza programu hiyo jambo ambalo litaisaidi Taasisi hiyo kutambua vipaumbe vya Zanzibar na hatimae kurahisisha utekelezaji wa programu hiyo.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo ya Sera na Utafiti ya Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasimi Natasha Ridge, ameeleza kuwa Taasisi hiyo pia, inajishughulisha na utoaji wa mafunzo ya kitaalamu ya kuwajengea uwezo walimu kuanzia ngazi ya Msingi hadi Sekondari.

Hata hivyo uongozi wa Taasisi hiyo uko tayari kuja Zanzibar mnamo mwezi wa Novemba mwaka huu kwa ajili ya kukutana na uongozi wa Wizara ya Elimu pamoja na uongozi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ili kuangalia vipaumbelea ambavyo wao wataweza kuvifanyia kazi katika kutoa mafunzo hayo.

Categories
Z! Extra

Wawili wazuiliwa na polisi kwa kuwaua watoto waliofanya ‘haja kubwa hadharani’

Roshini, 12 na Avinash 10 walishambuliwa siku ya Jumtano walipopatikana wakifanya haja kubwa karibu na barabara moja ya kijijini, walisema.

Familia ya watoto hao waliambia BBC Hindi kwamba hawana vyoo nyumbani. Mamilioni ya raia wa India hufanya haja kubwa hadharani swala ambalo huwaweka watoto na wanawake hatarini.

Dalits wapo katika mfumo wa chini wa Hindu na licha ya kuwa na sheria za kuwalinda, wanakumbwa na ubaguzi nchini India.

”Watoto hao wawili walipigwa hadi kufa na fimbo”, afisa wa polisi Rajesh Chandel aliambia mwandishi wa BBC Shuraih Niazi.

“Tumewawekea shtaka la mauaji wote wawili. wanahojiwa”. Saa chache baada ya shambulio hilo siku ya Jumatano asubuhi , maafisa wa polisi waliwakamata wanaume wawili – Rameshwar Yadav na Hakim Yadav.

Roshni na Avinash walikuwa binamu , lakini Roshni alikuwa amelelewa na wazazi wa Avinash na kuishi nao. Babake Avinash, Manoj, anasema kwamba kama mfanyakazi wa kila siku , hana uwezo wa kujenga choo katika nyumba yake.

Pia anasema kwamba ameshindwa kupata ruzuku ya serikali kama mpango wa kuwajengea vyoo watu masikini. Programu ya Swachh Bharat Mission au mpango wa usafi wa India unataka kumaliza haja kubwa za hadharani na kuimarisha usafi nchini humo.

Wakati waziri Mkuu Narendra Modi alipozindua mpango huo mnamo 2014, aliapa kuifanya India kuwa eneo la kufanya haja kubwa hadharani kufikia 2 Oktoba 2019. Kijiji cha Manoj – Bhavkhedi – kimetangazwa “kuwa kijiji ambacho hakina watu wanaofanya haja kubwa hadharani , jina mbalo serikali imekuwa ikivipatia vijiji na miji ambayo imefanikiwa kuzuia haja kubwa hadhrani.

Utafiti umeonyesha kuwa huku ujenzi wa vyoo ukiongezeka kwa kasi kubwa , ukosefu wa maji, utunzaji duni na mabadiliko ya polepoole ya tabia yamekuwa kikwazo kikuu cha kumaliza tatizo hilo.

Lakini wengi wamempongeza Bwana Modi kwa kuangazia suala hilo na kuzindua mpango huo mkubwa – ambapo wakfu wa Bill na Melinda Gates ulimtuza wiki hii , akielezea ujumbe huo wa Swachh Bharat kama “mfano kwa nchi zingine ulimwenguni ambazo zinahitaji kuboresha haraka kufikia huduma za maji safi miongoni mwa watu maskini duniani.”

Categories
Z! Extra

Wanawake waandamana kuiomba serikali iwatafutie waume

Amini usiamini Nigeria ina upungufu wa wanaume wa kuoa!! Kiasi kwamba wanawake wanaotamani kupata wenza na kutengeneza familia wameamua kuchukua hatua. Zaidi ya wanawake elfu 8 walio single wiki iliyopita waliandamana kutokana na upungufu wa wanaume wa kuwaoa.

Lengo la maandamano yao ni kuishinikiza serikali kuwasaidia waolewe, kivipi? (Ndio swali hata mimi nimejiuliza!)

Wanawake waliojikusanya na kuandamana ni mkusanyiko wa 5380 waliopewa talaka, 2200 ni wajane 1200 yatima, na 80 wengine. Wanawake hao wamedai kuwa hawana uwezo hata wa kununua chakula cha siku kwa sababu hawana wanaume wa kuwasaidia

Categories
Z! Extra

KESI YA KUVULIWA UBUNGE LISSU ITAANZA KUSIKILIZWA KESHO

Kesi ya kupinga kuvuliwa ubunge iliyofunguliwa na aliyekuwa mbunge wa zamani wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, inatarajiwa kuanza kusikilizwa kesho.


Hati ya kuwaita pande mbili imetolewa jana na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ikiwaita wahusika kufika katika shauri hilo linalosikilizwa mbele ya Jaji Sirilius Matupa.
Lisu amefungua shauri hilo chini ya hati ya dharura, kupitia kwa kaka yake Wakili Alute Mughwai, ambaye amempa mamlaka ya kisheria kufanya hivyo.

Katika hati ya dharura, Lissu anaiomba mahakama hiyo isikilize na kutoa uamuzi wa maombi yake haraka kwani vinginevyo, Mtaturu ambaye alitangazwa na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, ataapishwa kushika wadhifa huo.
Hivyo anadai atakuwa ameathirika kwa kuwa atapoteza haki zake zote, kinga na masilahi yake yote yanayoambatana na wadhifa wake huo wa ubunge.

Categories
Z! Extra

Meli ya Mt. Mkombozi II yawasili Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa ahadi aliyoitowa kwa wananachi wa Zanzibar kununua meli mpya ya mafuta MT MKOMBOZI II imetimia ambapo meli hiyo imewasili Zanzibar ikitokea Shanghai nchini China.

Rais Dk. Shein akiwa Ofisini kwake Ikulu mjini Zanzibar alipata fursa ya kuiona meli ya MT MKOMBOZI II ikiwasili kutoka ukingoni mwa pwani ya Zanzibar ikitokea usawa wa kisiwa ch Chumbe na kuelekea katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja ilipokwenda kutia nanga.

Akiwa katika faranda ya jengo la Ikulu mjini Zanzibar Rais Dk. Shein alionekana akiwa na furaha kubwa wakati akiiangalia meli hiyo ikiwasili ikiwa ni kutokana na ahadi aliyoitoa na azma yake juu ya ujio wa meli hiyo mpya ya mafuta.

Meli hiyo iliyotengenezwa na Kampuni ya Damen Shipyard ya nchini Uholanzi imewasili rasmi katika Bandari ya Malindi Zanzibar majira ya saa saa tano za asubuhi na kupata mapokezi ya aina yake.

Wafanyakazi wa Wizara hiyo na viongozi wao pamoja na wafanyakazi wa taasisi nyengine za Serikali na sekta binafsi waliungana pamoja na baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika eneo la Bandari ya Malindi mjini Zanzibar kwa ajili ya mapokezi ya meli yao hiyo.

Mapema Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, mawasiliano na Usafirishaji Mustafa Aboud Jumbe akitoa taarifa kwa wananchi huko ofisi kwake Kisauni, amethibitisha ujio wa meli hiyo na kueleza jinsi hatua mbali mbali zilizochukuliwa katika mchakato wa kununuliwa meli hiyo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hadi kuwasili kwake hapa nchini.

Katibu Mkuu huyo amesema kuwa meli mpya MT UKOMBOZI II, ni meli mpya ambapo majadiliano juu ya ujenzi wa meli hiyo yalianza mwaka 2017 na mkukuku wake uliwekwa rasmi mwezi Julai mwaka 2018 na hatimae meli hiyo ujenzi wake ulimalizika mwezi April mwaka huu
2019.

Jumla ya Dola za Marekani 30.4 zilitumika kutengenezea meli hiyo ambapo ujenzi wake hadi kukamilika ulichukua miezi 18 ambapo meli hiyo ya MV MAPINDUZI II ina uwezo wa kuchukua abiria 1200 pamoja na tani 200 za mizigo.

Categories
Z! Extra

Barrack Obama akosoa viongozi wenye kutoa kauli za kibaguzi na chuki

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama amewataka Wamarekani kukataa lugha za chuki na kibaguzi kutoka kwa viongozi wao.

Obama amekuwa akiongea kwa nadra tangu alipoondoka madarakani, na japo hakumtaja kiongozi yeyote kwa jina, lakini kauli yake hiyo imekuja baada ya rais Donald Trump akiwa katika harakati za kujinasua kuwa kauli zake dhidi ya wahamiaji ndizo chanzo cha kuchochea mauaji nchini humo.

Katika hotuba yake jana Jumatatu, Trump alikemea ubaguzi wa rangi. Jumla ya watu 31 wameuawa katika mashambulio ya bubduki kwenye majimbo ya Texas na Ohio mwishoni mwa wiki.

 

Akiwa madarakani, Obama alipigana pasi na mafanikio kudhibiti umiliki wa silaha za moto nchini Marekani. Aliiambia BBC mwaka 2015 kuwa, kushindwa kupitisha kwa sheria za kudhibiti silaha ndilo jambo kubwa alilofeli akiwa kama kiongozi wa nchi hiyo.

Trump kulipa kisasi kwa ”upumbavu”wa Macron Mkuu wa ujasusi Marekani ajitenga na utawala wa Trump. Obama amekuwa akikwepa kuzungumzia sera za Trump, hususani ya uhamiaji ambayo imekuwa ikipingwa na makundi tofaouti, hata hivyo, safari hii ametoa tamko.

“Inabidi kwa pamoja tukatae lugha zinazotoka kwenye kinywa cha kiongozi wetu yoyote ambaye analisha mazingira ya uoga na chuki ama anayefanya ubaguzi kuwa jambo la kawaida. Viongozi ambao wanawafanya watu ambao hawafanani nasi kuonekana kama mashetani, ama wanaodai kuwa watu wengine ikiwemo wahamiaji wanahatarisha mfumo wetu wa maisha, ama wanaodai kuwa Marekani ni ya jamii moja tu ya watu,” amesema Obama.

Categories
Z! Extra

Balozi Seif Ali Iddi amesema elimu itolewe kwa viongozi wachanga

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Viongozi wakuu wanajukumu la kuwaelimisha viongozi wachanga juu dhana halisi ya uwezo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar .


Balozi Seif Ali Iddi amesema hayo Ofisini kwake Vuga wakati akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayesimamia Muungano na Mazigira George Simbachawene aliyefika kujitambulisha baada ya Kuteuliwa Hivi karibuni kushika Wadhifa huo.

Amesema kazi kubwa inayokabili Watanzania kwa wakati huu ni kuendelea kuuimarisha Muungano huo ulioleta faida kubwa Kiuchumi na Ustawi wa Jamii, faida ambayo inaweza kuwa funzo zuri la kuigwa na Mataifa mengine.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amemuhakikishia Waziri Simbachawene kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na Ofisi yake katika Kazi kubwa iliyo mbele ya kuona Umoja na Mshikamano uliojengeka kupitia Muungano huo inaimarika na kustawi kwa maslahi ya Wananchi wote.

Mapema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayesimamia Muungano na Mazigira George Simbachawene amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar una shabaha Maalum iliyopelekea Waasisi wa Taifa hili kufikia mamuzi ya Kuunganisha Mataifa Mawili yaliyo Huru.

Categories
Z! Extra

Nchi za Jumuiya ya SADC, zimeobwa kupeana fursa wenyewe kwa wenyewe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amezitaka nchi za Jumuiya ya SADC, kupeana fursa wenyewe kwa wenyewe hasa linapofikia suala la biashara na kuziomba nchi hizo, kuangalia namna ya kushirikiana kwa manufaa ya uchumi wa viwanda.

Ametowa agizo hilo wakati akifungua maonesho ya viwanda ya nchi za Jumuiya ya SADC, yaliyofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Rais magufuli amesema ni busara kama jumuiya itaweka kipaumbele kwenye utumiaji wa teknolojia ya viwanda kabla ya kwenda mbali na kuuziana bidhaa kabla ya kwenda kwingine, kama nchi ya jumuiya watapohitaji bidhaa kuwapelekee, ili soko la watu Mil. 300 wa SADC kukuza uchumi.

Maonesho hayo ya viwanda yanatarajia kufanyika kwa wiki nzima kuanzia august 05, ambapo mara baada ya kukamilika kwa maonesho hayo, utaanza mkutano wa Marais 19 wa nchi za Jumuiya ya SADC ambapo Rais Magufuli ni Mwenyekiti.

Categories
Z! Extra

Mwandishi habari Tanzania Erick Kabendera amepandishwa kizimbani


Mwandishi habari Tanzania Erick Kabendera amepandishwa kizimbani kusomewa mashtaka mapya matatu ya ubadhirifu wa kiuchumi .

Katika mashtaka hayo Kabendera anatuhumiwa na kujihusisha na genge la uhalifu na uhujumu wa uchumi nchini kukwepa kulipa kodi ya zaidi ya milioni mia moja za kitanzania.

Kosa la tatu ni la utakatishaji fedha zenye thamani ya zaidi ya millioni mia moja na sabini.
Kwa mujibu wa mashtaka yaliowasilishwa, Kabendera anadaiwa kuyatekeleza hayo baina ya Januari 2015 na Julai mwaka huu mjini Dar Es Salaam na kwa baadhi ya makosa anadaiwa kuyafanya kwa ushirikiano wa watu ambao hawakuwepo mahakamani leo.

Makosa yote hayana dhamana.


Mawakili wake wameondoa ombi la dhamana kutokana na mashtaka hayo mapya.

Akizungumza na waandishi habari punde baada ya Kabendera kusomewa mashtaka, wakili wake Jebra Kambole amesema

‘Wakati Erick anakamatwa siku ya kwanza aliambiwa kosa lake ni la uhamiaji, akapelekwa kwenye mamlaka za uhamiaji, akahojiwa, pasipoti yake ikachukuliwa. Uhamiaji wakamkabidhi kwa jeshi la polisi makao makuu Central Jeshi la Polisi wakamhoji kwa makosa ya uchochezi.

‘Kuanzia hapo hajawahi kuhojiwa kwa makosa mengine zaidi ya hayo’ amesema Jebra Kambole.

Amefafanuwa kwamba kutokana na kwamba mashtaka aliyosomewa Kabendera hayana, dhamana ameshindwa kutoka leo.
‘Tunachofanya sasa, ni kuangalia upelelezi unafanyika kwa wakati’ ameeleza Wakili huyo.

Kesi dhidi ya Erick Kabendera inatarajiwa kusikilizwa Agosti 19.
Erick Kabendera mwandishi habari anayeandika magazeti ya ndani na nje ya Tanzania alikamatwa Jumtatu 29 Julai wiki iliopita na watu waliojitambulisha kuwa ni maafisa wa polisi.

Katika mkutano na vyombo vya habari, kamanda wa polisi kanda maalum ya mji wa Dar Lazaro Mambossasa amesema kuwa mshukiwa huyo alikaidi agizo la polisi la kufika mbele yao kwa ajili ya mahojiano.

”Mwandishi huyu aliitwa hakutekwa lakini kwa ujeuri alikaidi wito huo…. kimsingi pengine iwapo angewasili angehojiwa na kuachiliwa”, alisema Mambossasa

Categories
Z! Extra

WAZIRI WA ARDHI TANZANIA ATOA ONYO

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, leo Agosti 3, amemrejeshea kiwanja Brigedia Mstaafu Fransis Mbenna, kilichopo Mbezi Beach DSM alichodhulumiwa kwa takribani miaka 20. Pia ametoa onyo kwa baadhi ya wanasheria wanaochelewesha kesi kwa makusudi