Categories
Photos

Siku ya 5: Angalia picha za matukio mbalimbali katika Tamasha la ZIFF

Ikiwa zimesalia siku kadhaa kuendea mwishoni mwa tamasha la filamu za nchi za majahazi (ZIFF), kwa siku ya jana (Jumatano, Julai 12) wananchi wengi walihudhuria katika tamasha hilo ambapo walianza kuangalia filamu na baadae kuhamia kwenye upande wa burudani.

Mohammed Issa Matona ndie ambae aliyetoa burudani kwa usiku wa jana na kikundi chake cha G Clef band ambapo kilisindikizwa na wanamuziki maarufu mbali mbali kutoka Tanzania kama vile Makame Faki, Mohammed Ilyas, Spider Bashan na wengine wengi.

Angalia picha hapo chini ujionee.

This slideshow requires JavaScript.

Categories
Photos

Picha: Ufunguzi wa Tamasha la ZIFF 2017

Siku ya Jumamosi tarehe 8 Julai, ilikuwa ni siku ya kutimiza miaka 20 ya Tamasha la Filamu za nchi za majahazi Zanzibar (ZIFF) ambapo ufunguzi wake ulifanyika katika ukumbi wa Ngome Kongwe.

katika ufunguzi huo kulihudhuriwa na wageni kutoka nchi mbali mbali ambapo mgeni rasmi katika tamasha hilo alikuwa ni raisi mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe Jakaya Mrisho Kikwete.

Baada ya ufunguzi wa Tamasha, filamu ya T-Junction ndio ilikuwa ya kwanza kuonyeshwa ambayo iliyotengenezwa na waongozaji kutoka Tanzania kama Amil Shivji na wengineo.

Kauli mbiu ya tamasha hilo Kujisiki furaha ambalo litaendelea mpaka tarehe 16 Julai.

Angalia picha za ufunguzi huo.

This slideshow requires JavaScript.

 

Categories
Photos

Picha: Rico Single alivyotoa burudani Full Moon Party Wikiendi hii

Msanii wa muziki Rico Single aliweza kuzifurahisha nyoyo za wageni mbali mbali waliofika katika Full Moon Party iliyofanyika siku ya Jumamosi (Machi 11) katika ufukwe wa Kendwa Rocks iliyopo Nungwi, Zanzibar.

Katika onyesho hilo lilifunguliwa na kikundi cha ngoma za asili na kufuatiwa na Muimbaji kutoka Jamaica, Pampi Judah ambaye alitoa burudani ya raggae vizuri na baadae kufuatiwa na Rico Single aliyepanda kwenye steji na Live band.

Angalia picha za onyesho hilo lilivyokuwa

This slideshow requires JavaScript.

Categories
Photos

Picha: Rico Single, Bob Maghrib & Batimbo walivyotoa burudani kwa wageni katika Tamasha la Sauti za Busara

Ikiwa imebakia siku moja kuendea tamati, wasanii kutoka nchi za mbali mbali za Afrika walitoa burudani katika tamasha la Sauti za Busara kwa wageni mbali mbali walioshiriki katika viwanja vya Ngome Kongwe Zanzibar.

Wasanii kama Bob Maghrib (Morroco), Rico & The Band na Batimbo Percussion Magique kutoka Burundi, walitoa burudani ya kutosha na kuweza kulipamba vizuri tamasha kwa siku hiyo.

Angalia picha hapo chini (Picha zote: Othman Maulid)

This slideshow requires JavaScript.

Categories
Photos

Picha: DJ Waiz ashoot video ya ‘Shobo Robo’

Hatimaye msanii na mwanamitindo wa muda mrefu, DJ Waiz ameshoot video ya wimbo wake mpya ‘Shobo Robo’ ambayo alioshirikiana na Baby Jay na Kijukuu.

Akiongea na Zenji255, Waiz amesema kuwa kwa kipindi kirefu alikaa kimya ni kutokana na majukumu ya mitindo kuwa mengi na kwa upande wa muziki ilimbidi ayasome mabadiliko yaliyokuwepo katika muziki ili ajue anarudi kwa ‘style’ gani.

“Muziki kiukweli umekuwa hivi sasa kwa hapa kwetu, vijana sasa hivi wameamka sana kimuziki na ndio maana nikaamua nirudi kwa presha ya hali ya juu kuanzia wimbo mpaka video” Amesema DJ Waiz.

Video ya wimbo huo imetayarishwa na Director Pablo na imetumika siku tatu kuitengeneza video hiyo, na katika video wanamitindo mbali mbali walishirikishwa akiwemo Chidy Adore na wengine wengi. Video inatarajiwa kuachiwa wiki moja kuanzia sasa.

Picha kwa msaada: Chiwile Jr.
Categories
Photos

Picha: Siti & The Band, Ison Mistari, Kali na Asali walivyotoa burudani katika uzinduzi wa video ya ‘Nani nilimkosea’

Siku ya Jumapili (Feb .5) Ilikuwa ni usiku wa uzinduzi wa video mpya ya ‘Nani Nilimkosea’ ya rapa Ison Mistari.

Kiukweli watu wengi walifurahi Mapinduzi ya uzinduzi huo. Burudani nyingi zilifanyika, wasanii na wadau mbali mbali wa burudani walihudhuria katika uzinduzi huo. Vikundi vya burudani kama Wakushi band, Kali na Asali, Siti & The Band, Alfa na Ison Mistari walitoa burudani katika shuhuli hiyo.

Angalia picha jinsi uzinduzi huo ulivyokuwa.

This slideshow requires JavaScript.

Categories
Photos

Picha: Rahatul-Zaman na Smile walivyotoa burudani katika uzinduzi wa ‘The Dream’

Usiku wa jana (Jan. 28) kikundi cha taarab asili cha Rahatul-Zaman na msanii wa kizazi kipya Smile, walitoa burudani katika uzinduzi wa filamu mpya ya ‘The Dream’ katika ukumbi wa Ngome Kongwe Zanzibar.

Hii ni mara ya kwanza kwa tasnia ya filamu hapa visiwani kufanyika uzinduzi kama huu ambapo mgeni rasmi wa usiku huo alikuwa mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Ayoub Mohammed na walihudhuria wageni mbali mbali akiwemo mwakilishi wa jimbo la Kikwajuni Al-Jazeera.

Katika uzinduzi kulikuwa na ugawaji wa vyeti kwa wadhamini mbali mbali waliosaidia kufanikisha filamu hiyo mpaka ikakamilika vile vile kulifanyika mnada wa kuiuza CD ya filamu hiyo pamoja na vikombe na pia Mkuu wa mkoa alipatiwa zawadi ya vibuli kutoka Rwanda.

Angalia picha za uzinduzi huo hapo chini

This slideshow requires JavaScript.

Categories
Photos

Picha: King Majuto na Kingwendu walivyowavunja mbavu watoto Kariakoo

Ikiwa ni siku ya kusherehekea siku ya Mapinduzi ya Zanzibar, Januari 12. Wachekeshaji kutoka Tanzania Bara, King Majuto na Kingwendu Ngwendulile walitoa burudani ya vichekesho kwa watoto waliotembelea viwanja vya kuchezea watoto Kariakoo.

Katika viwanja hivyo kulihudhuriwa na watu wa rika la kila aina, kuja kuwaona wasanii wakitoa burudani hiyo iliyodhaminiwa na Mtandao wa Zantel.

Categories
Photos

Picha: Wasanii wa Zenji Fleva walivyopamba Mkesha wa siku ya Mapinduzi Maisara

Chama cha wasanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Zanzibar jana (Januari 11) kilitoa burudani katika mkesha wa kuadhimisha siku ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwapandisha wasanii wao mbali mbali kutoka Zanzibar.

Katika shamra shamra za mkesha huo uliohudhuriwa na viongozi mbali mbali pamoja mamia ya wazanzibari waliokuja kuangalia burudani hiyo.

Angalia picha za mkesha huo

Categories
Photos

Picha: DJ Khaled anunua jumba la kifahari la Beverly Hills $9.9 Milioni

Msanii kutokea nchini Marekani, DJ Khaled ameinunua nyumba ya kifahari ya Beverly Hills iliyokuwa ikimilikiwa na muimbaji na muigizaji maarufu Robbie Williams kwa dola millioni 9.9za kimarekani, Kwa mujibu wa mtandao wa Variety.

Nyumba hiyo ya kifahari ilimilikiwa na Robbie toka mwaka 2002 ambapo aliinunua kutoka kwa mwanamuziki wa miondoko ya Country Clint Black na muigizaji wa kike Lisa Hartman kwa dola Million 5.45.

Angalia picha za nyumba hiyo ya kifahari kwa ndani

 

Categories
Photos

Picha: Blue, Barnaba na Linex walivyopagawisha Zanzibar

Usiku wa kuamkia Jumamosi Disemba 3,Wasanii kutoka Dar es Salaam Mr. Blue, Barnaba na Linex walifanya onyesho la kufungia mwaka katika ukumbi wa CCM Maisara.

Katika onyesho hilo msanii Jumaa Town alifungua show hiyo akiwa na ‘madancer’ wake ambapo mzuka uliwapanda madancer hao na kuvunja steji ambalo walilokuwa wakilitumia kwa ajili ya onyesho lao.

Baada ya hapo ilifuatiwa na Live Band kutoka kwa Barnaba na Linex na mwisho Mr Blue alimalizia onyesho hilo.

Categories
Photos

Picha: Penny Royal wapewa tunzo ya uchangiaji bora kwenye Taasisi ya Siti Bint Saad

Taasisi ya Siti Bint Saad hapa Zanzibar iliwakabidhi tuzo na zawadi mbali mbali kwa muekezaji wa Penny Royal kwa mchango wake mkubwa kufanikisha Ujenzi wa Jengo la Kumbukumbu ya Siti Bint Saad linalotarajiwa kujengwa katika Kijiji ambapo mwanamuziki huyo alipozaliwa kilichopo Fumba Zanzibar.

Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Bi Nasra Mohammed Hilal alimkabidhiwa kadi ya Uanachama wa Taasisi hiyo No 20. Hafla hiyo iliofanyika katika Ofisi za PennyRoyal Mazizini Zanzibar.

1 2 3 4 5 6 7 8 9 10

Categories
Photos

Picha: Teyana Taylor na Travis Scott wakava jarida la Paper

Mwanadada kutoka Marekani Teyana Taylor akiwa rapa Travis Scott wamekava katika toleo jipya la jarida la Paper.

paper-mag-october-1 paper-mag-october-2 paper-mag-october-3 paper-mag-october-4 paper-mag-october-5 paper-mag-october-6 paper-mag-october-7 paper-mag-october-9

Categories
Photos

Picha: Show ya Lady Jay Dee ‘Naamka Tena Tour’ Intebe

Wikiendi hii mwanadada na mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva Lady Jay Dee alifanya ziara yake visiwani Zanzibar ikiwa ni moja ya ‘Naamka Tena’ iliyofanyika katika ukumbi wa Intebe.

Angalia picha za show hiyo

1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14

Categories
Photos

Picha: Tamasha la kuchangia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera

Wasanii wa muziki wa Bongo Fleva wameibuka washindi kwa penati tano kwa nne dhidi ya wasanii wa Bongo Movie katika mechi ya hisani kwa ajili ya kuwachangia waathirika wa tetemeko la ardhi Bukoba.

Katika mechi hiyo iliyofanyika uwanja wa Taifa ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, ambayo ilikuwa na ushabiki mkubwa kwani wasanii wa Bongo fleva waliungana na wasanii kutoka Zanzibar na kuweza kufanya timu yao kuibuka na ushindi wa penalti 5 kwa 4. Awali hapo mwanzo mechi hiyo ilimaliza 1-1 ambapo goli la Bongo Movie lilifungwa na Mteze na H.Baba dakika chache baadae akasawazisha.

Katika mechi nyingine kati ya wabunge wa Yanga na wabunge wa Simba, wabunge wa Yanga waliondoka na ushindi baada ya kuwafunga wabunge wa Simba goli 5 kwa 2.

Angalia picha za matukio mbalimbali.

img_7906 img_7907 img_7933 img_7942 img_7950 img_7951 img_7954 img_7980 img_7982 img_8000 img_8002 img_8014 img_8015 img_8030 img_8032 img_8035 img_8038 img_8042 img_8047 img_8063 img_8075 img_8079 img_8087 img_8094 img_8096 img_8119 img_8131 img_8177 img_8184 img_8194 img_8266 img_8286

Categories
Photos

Picha: Msimu mwingine wa Tamasha la Jahazi Jazz visiwani Zanzibar

Msimu mpya mwingine wa tamasha maarufu kwa muziki aina ya jazz, Jahazi Literary & Jazz Festival mwaka huu umerudi tena na wasanii mbali mbali kutoka nchi tofauti barani Afrika na kwengineko.

Wasanii kama Carl Winters, Christine Kamau kutoka Kenya, Ida Neilson Fathy Salama na wengine wengi walipamba ufunguzi wa tamasha hapo jana katika ukumbi wa Ngome Kongwe Zanzibar.

Angalia picha za ufunguzi wa tamasha hapo chini

Carl Winters na Anna Paulina
Carl Winters na Anna Paulina

2

Chritine Kamau kutoka Kenya
Chritine Kamau kutoka Kenya

5

Morten Schanz Quartet
Morten Schanz Quartet

8 15 14 12

Categories
Photos

Picha: Wanne Star na Michael Jackson wa Zanzibar walivyotoa burudani Nungwi

Wikiendi ilianza uzuri kwa baadhi ya kumbi za hapa visiwani ambapo vikundi na wasanii mbali mbali waliweza kutoa burudani za kila aina katika sehemu tofauti.

Kwa Upande wa mji wa Nungwi katika hoteli Mocco Beach Villa, Kendwa. Kikundi kilichopata umaarufu sana nchini Tanzania kwa kucheza ngoma za asili pamoja na kucheza na nyoka waliweza kutoa burudani ya kufa mtu ambapo walisindikizwa na dancer anayecheza miondoko kama ya Michael Jackson.

Angalia burudani hiyo ilivyokuwa

4

5

6

2

3

1

Categories
Photos

Picha: Kupokelewa na Kuzikwa kwa mwili wa Marehemu Aboud Jumbe

Mwili wa aliyekuwa Raisi wa awamu ya pili Zanzibar, Marehemu Aboud Jumbe amezikwa jumatatu Agosti 15 visiwani Zanzibar nyumbani kwake Migombani.

Viongozi mbali mbali walihudhuria katika mazishi hayo akiwemo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Mhe. Dk Ali Mohammed Shein.

Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi alishika wadhifa wa Rais wa Zanzibar April 7, 1972 mara baada ya kifo cha aliyekuwa rais wa kwanza wa Zanzibar Abeid Amani Karume.

Hayati Aboud Jumbe alijiuzulu urais wa Zanzibar pamoja na nyadhifa nyingine za makamu mwenyekiti wa CCM na makamu rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Januari 30, 1984.

Marehemu amefariki akiwa na umri wa miaka 96 ameacha watoto 13, na wajukuu 40, Mwenyezi ailaze roho ya marehemu popeni Amina.

1 3 4 5 6 8 9 10 11 12 14

Categories
Photos

Picha: Maelfu wajitokeza kuuaga mwili wa Bondia Muhammad Ali

Bondia Maarufu Muhammad Ali maelfu ya watu walijipanga barabarani ili kumuaga wakati msafara ukipita kuelekea mji wa kwao Louisville, Kentucky ambapo ndo alipo zikwa June 10 2016.

Watu maarufu mbalimbali walikuwepo katika mazishi hayo ya Muhammad Ali akiwemo Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton,Promoter Don King,David Beckham,Arnold Schwarzenegger,Lennox Lewis, Will Smith, John Grady and Mike Tyson.

1 2 3 4 5 6 7 8 9 10Chanzo: Bongo5

Categories
Photos

Picha: Uzinduzi wa Baraza la Vijana, Jimbo la Kwahani

IMG_6862 IMG_6865 1 2 3 4 IMG_6852 IMG_6856 IMG_6858