Siti Amina akiwa amewashirikisha Vanito na Richard kwenye gita amekuletea wimbo mpya unazungumzia ugonjwa hatari wa Corona. Wimbo unaitwa “Homa ya Dunia” umetayarishwa na producer Razakey kutoka studio za Island Records Zanzibar.
Umoja wa wasanii wa muziki wa kizazi kipya Zanzibar Flava Unit wameachia wimbo mpya ambao unaozungumzia dhidi ya ugonjwa hatari wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya Corona.
Akizungumza na Zenji255 Raisi wa ZFU Laki, amesema kuwa kutengeneza wimbo huo kwetu tumeona ni vizuri ili kuweza kuhamasisha jamii yetu ya Zanzibar na duniani kwa ujumla juu ya kujikinga na virusi vya Corona.
“Kiukweli virusi vya Corona vinasambaa kwa haraka sana, na kwa hapa tulipofikia sasa inabidi jamii ikae katika uangalizi mzuri. Kwanza, kujikinga. Pili, kuelemisha. Na ndio maana tukaamua kukaa chini na kutengeneza wimbo huu ambao ni burudani, lakini ndani yake kuna ujumbe wa kuhusu virusi hivyo” Raisi Laki.
Katika wimbo huo wameshiriki wasanii kama Nedy Music, Baby J, Chaby Six, Abramy, Zenji Boy, Sultan King, Rico Single, Sapna, Pozza Boy, Smile, Yoram na Laki wa Promise.
Wimbo mpya kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya Abramy the Voice unaitwa “Naumia”. Wimbo umetayarishwa na producer Alex Chata kutoka studio za Dynamic.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Wiz D ameufungua kwa kuachia wimbo wake mpya unaitwa “Hapo” akiwa amemshirikisha mwanadada Taly. Wimbo umetayarishwa na producer Bonge Jr. kutokea studio za Furaha Records.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Sharo Music ameachia wimbo wake mpya unaitwa “Download”. Wimbo umetayarishwa na producer Bonge Jr. kutoka studio za Furaha Records.
Msanii wa kike wa kizazi kipya Rayna ameachia wimbo wake mpya unaitwa “Nitazoea”. Wimbo umetayarishwa na producer Dapro kutokea Blueprint Music Station.
Wimbo mpya kutoka msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka visiwani T.I.P King ameachia wimbo wake mpya unaitwa “Noma Noma” akiwa amemshirikisha Junid J, Extra na Wiz Israal. Wimbo umetayarishwa na producer Bonge Jr.
Baada ya kimya kirefu, msanii wa muziki wa kizazi kipya kutokea visiwani Cool Kaka ameachia wimbo mpya unaitwa “Kidume”. Wimbo umetayarishwa na producer Bab Chiddy kutokea Most Wanted Studios.
Wimbo mpya kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya kutokea visiwani Zanzibar, Muslee wimbo unaitwa “Alele”. Wimbo umetayarishwa na producer Chilly K katika studio za Action Music.
Kutokea visiwani Zanzibar, wimbo mpya kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya Rico Single. Wimbo unaitwa “Bend Over”, akiwa amewashirikisha Smile The Genius na Black. Wimbo umetayarishwa na producer na Aloneym katika studio za Island Records.
Wimbo mpya kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya Aley Star unaitwa “Makorora” akiwa amemshirikisha Mapanch BmB. Wimbo umetayarishwa na producer Kimambo.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Alatish Mabawa ameachia wimbo wake mpya unaitwa “Kipepeo” akiwa amemshirikisha Sultan King, wimbo umetayarishwa katika studio za Action Music na producer Chilly K.
Wimbo mpya kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya Polandy TheGenius, wimbo unaitwa “Sauna” akiwa amemshirikisha Hemedy Music. Wimbo umetayarishwa na producer Stoppa kutoka studio za MK Records.
Kwa muda mrefu wasanii waliokuwa wakifanya kazi kwa pamoja chini ya mwamvuli wa wavanilla kabla ya kuvunjika Abramy na Smile wasaniii hawa hawakufanya kazi ya pamoja kwa muda mrefu sasa wamekuja na wimbo mpya uitwao kunywa wimbo umetayarishwa katika kiwanda cha muziki serious music chini ya mtayarishaji Chidy Master
sikiliza kisha tupe maoni yako je unadhani kunahaja ya wavanilla kurudi