Categories
E! News

Mwana FA na Sallam SK wathibitisha kuwa na maambukizi ya COVID19 (Corona)

Mwanamuziki wa Bongo Flava nchini Tanzania, Hamisi Mwijuma, maarufu Mwana FA ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa amegundulika kuwa ameathirika na virusi vya COVID- 19 au corona.

FA amesema alifanya vipimo hapo jana na kupatiwa majibu yake hii leo vilivyobainisha kuwa ameathirika na virusi hivyo.

Katika kipande chake cha video alichokiweka kwenye mtandao huo, Mwana FA alieleza kwenye ukurasa wake kuwa alitoka Afrika Kusini juzi na kubaini kuwa joto lake la mwili halikuwa la kawaida.

”Sababu ya kufanya hivyo nilikuwa natoka safarini Afrika Kusini, joto langu la mwili lilikuwa halieleweki, linapanda, linashuka hivyo nilivyorudi kwa sababu habari duniani inayofahamika ni hiyo nikawa nimejitenga ili kuhakikisha siwaathiri watu wengine”.

Mwanamuziki huyo amesema kwa sasa ile homa aliyokuwa akiihisi juzi kwa sasa haipo tena lakini bado amejitenga wakati afya yake ikiendelea kuimarika.

Awali mbali na mwanamuziki huyu pia menaja wa Diamond Sallam SK naye pia amethibitisha kuwa na virusi vya corona lakini mpaka sasa amesema anaendelea vizuri.

Categories
E! News

Sauti za Busara 2020 na kampeni dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia kwenye muziki

Wasanii wengi wa kike barani Afrika na kwingineko huendelea kupambana na unyanyasaji wa kijinsia katika tasnia ambayo inaendelea kubaki chini ya mfumo dume. Waathirika wa dhulma hizi mara nyingi huogopa kuongea kwa sababu matokeo yake yanaweza kuathiri kazi au maisha yao binafsi.

Hata wale ambao wanachagua kujitokeza kwa umma, maelezo yao hayachukuliwi kwa uzito na mamlaka kwa kuchukua hatua muhimu dhidi ya dhuluma kama hiyo. Mara nyingi kwa kuwa wana nafasi finyu, waathirika huishia kuacha mahali pa kazi au tasnia kwa jumla, lakini kwa wahusika maisha yao yanaendelea kama kawaida.

Mwaka huu katika tamasha la Sauti za Busara 2020 ambalo linatarajiwa hufanyika Mji Mkongwe, Unguja mnamo Februari 13 hadi 16, waandaaji wameamua kutilia mkazo swala hili kwa kauli mbiu inayosema ‘Pandisha Sauti Yako, Sema Hapana kwa Unyanyasaji wa Kijinsia.

Akiongea leo Yusuf Mahmoud, mkurugenzi wa tamasha hilo alisema lengo kuu la kampeni hiyo ni kubadili mitizamo, kuanzisha mazungumzo, na kuhamasisha heshima kwa wanawake kwa kuongeza uhamasishaji juu ya unyanyasaji wa kijinsia.

Anasema hii ni muhimu ili kuleta mabadiliko ya tabia na kwa sababu hiyo, ujumbe unaolenga suala hilo utafikia tamasha nzima kwa ujumla.

“Wasanii wengi wa tamasha, ndani na nje ya nchi wamekubaliana kuhakikisha kuwa kampeni hii inafanikiwa kuunganisha watazamaji wa tamasha hapa Tanzania na kwingineko, “alisema Yusuf Mahmoud.

Tamasha limeaanda shughuli zinazolingana za kukuza mifano ya jinsia, kama vile mafunzo ya usimamizi wa jukwa kwa wanawake, itakaoongozwa na mtaalamu kutoka Zimbabwe, Ushirikiano wa kisanii wa Swahili Envcounters, Circus4Life na vikundi vingine vya wanawake ambavyo vitashiriki kwenye gwaride la ufunguzi.

“Jukumu letu kuu kama waandaaji wa tamasha ni kusaidia kujenga ustadi na uwezo kwa watanzania katika tasnia ya muziki. Ninazungumzia wasaani wakiwa jukwani, na pia watu wengi nyuma ya pazia: wasimamizi, wazalishaji, sauti na mafundi wa taa na kadhalika.”

Aliongeza: “Hivi sasa nchini Tanzania, wanawake wachache ndio wanaojitokeza kuingia kwenye muziki wa asili na hii ndio sababu tamasha la Sauti za Busara 2020 tumealika wasanii kama Siti & the Band (Zanzibar), Thaïs Diarra na Mamy Kanouté (kutoka Afrika Magharibi), Pigment (Reunion), Evon na Apio Moro (Uganda). Wengine ni Circus4Life kutoka Bagamoyo, na na DJs kutoka Afrika Mashariki. Wote ni wanawake wenye shauku ambao hutumia muziki kuwasiliana na kujielezea. Wakati huo huo, wakitoa burudani nzuri!”

Yusuf Mahmoud aliongeza, “tamasha lina imani wasanii hawa wanaoshiriki watatoa msukumo, kutoa matumaini na motisho kwa wanawake na wasichana wengi ambao wanaweza pia kuzingatia kazi ya muziki.”

Tamasha la Sauti za Busara, 13 – 16 Februari 2020 linadhaminiwa na Ubalozi wa Norway, Africalia, ubalozi wa Uholanzi, Bristish Council, Zanzibar Media Corporation, Zanlink, Memories of Zanzibar Ubalozi wa Ufaransa, Emerson Zanzibar, Radio ya Chuchu FM, Mozeti, Music in Afrika na zaidi.

Categories
E! News

Producer Buju Mandevu afiwa na mama yake mzazi

Mama Mzazi wa mtayarishaji wa muziki kutokea visiwani Zanzibar, Abubakar almaarufu kama Buju Mandevu amefariki dunia leo Jumamosi Oktoba 12, 2019 akiwa nyumbani kwake maeneo Majestic ndani ya Mji Mkongwe.

Taarifa ya kifo hicho, imethibitishwa na familia ya producer na mipango ya mazishi yanatayarishwa na familia na taarifa itatolewa. Zenji255 inatoa pole kwa familia ya Buju Mandevu kwa msiba mzito alioupata na mungu atamfanyia wepesi katika kipindi hiki kigumu.

Endelea kufuatilia Zenji255 katika mitandao yetu kwa taarifa zaidi.

Categories
E! News

Picha: Smile The Genius achaguliwa kuwa balozi wa taulo za kike (Pedi)

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Smile the Genius amepata dili la kuwa balozi wa kugawa taulo za kike (Pedi) katika shule mbali mbali nchini Tanzania.
Smile alitangazwa rasmi jana na kampuni inayosimamia mradi huo ambapo amechaguliwa yeye na mchekeshaji maarufu nchini MC Pilipili, ambapo mradi huo ulifunguliwa rasmi katika wilaya ya Kisarawe mbele ya mgeni rasmi mkuu wa wilaya hiyo Jokate Mwegelo.
Akizungumza na Zenji255 Smile amesema kuwa kwa upande wake ameshukuru kwa heshima aliyopewa na kusema amekubali kuwa balozi wa mradi huo si kwa kuwa amepata dili ambalo litamlipa, lakini yeye anaichukulia kama harakati ya kuwakomboa watoto wa kike katika changamoto wanapokuwa katika masomo yao.
Zenji255 inatoa pongezi kwa msanii Smile kwa hatua aliyofikia. Angalia picha hapo chini Smile akiwa na Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mhe. Jokate Mwegelo.
Categories
E! News

Wiz D atembelea Ngorongoro, Arusha

Ikiwa ni moja ya kampeni ya Serikali ya jamhuri wa muungano ya Tanzania kuutangaza utalii wa ndani msanii wa muziki kutokea visiwani Zanzibar Wiz D ameamua kuwa mfano kwa Watanzania kwa kutembelea vivutio hivyo vya utalii.

Wiz D ambaye kwa sasa anafanya poa na wimbo ‘Body’ aliambatana na marafiki zake na  kutembelea katika mbuga ya wanyama ya Ngorongoro iliyopo mkoani Arusha.

Angalia picha za msanii huyo akiwa matembezi hayo mbugani hapo.

Categories
E! News

Fanny apata shavu la kufungua Fiesta Mwanza

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutokea visiwani Zanzibar, Fanny amepata nafasi ya kushiriki katika ufunguzi wa Tamasha la Fiesta linalosimamiwa na kampuni ya Clouds Media chini ya redio ya Clouds FM.

Kwa mwaka 2019 Fiesta itafanyika katika mkoa wa Mwanza na ambapo Fanny atakuwa katika list ya ufunguzi huo.

Akizungumza na Zenji255, Fanny amesema anafuraha kubwa sana kupata nafasi hiyo kwani kwa muda mrefu sana muziki wa Zanzibar kwenye tamasha la Fiesta haukusikika na kwa mkoa wa Mwanza ni pahala pake kuupeleka muziki wa Zanzibar.

“Hakuna kitu kizuri kama kuiwakilisha sehemu unayotokea unapokuwa ugenini, na mimi nafurahi sana kuwa nitakuwa wa kwanza kuutangaza muziki wa Zanzibar urudi katika ile nafasi yake ya zamani ambayo ilisahaulika kwa muda mrefu katika Fiesta” – Fanny

Fanny ameongeza kuwa “Nawaahidi wazanzibari na wasanii wenzangu kwamba sitowaangusha na nitahakikisha bendera ya Zanzibar inapepea kisawasawa. Kikubwa tupeane sapoti kwani hakuna kitu kizuri kama tukiwa pamoja na kushirikiana kupeleka muziki wetu duniani”

Categories
E! News

HARMONIZE AANDIKA BARUA YA KUOMBA KUVUNJA MKATABA WCB


Huwenda ndoto za watu waliokuwa wanatamani kuona Harmonize akitoka wcb zimetimia na huwenda ni kiini macho kauli ya SALAMI Sk kauli hii inanirejesha kwanye posti yetu tulio wahi kuposti takribani miezi miwili iliyopita.
bado nasema ningumu sana kwa konde kutoka wcb haya aliyosema salami kama nikweli basi jua nijambo la kibiashara na kunamtu anaandaliwa mazingira ya kupigwa vita mfano kama harmonize atatoka hii niwazi stori kubwa itakuwa kuizungumzia wcb na konde gang unapata picha yaani itakuwa imepoteza kuzungumzwa Diamond na Ali kiba na ikifika hapa sasa lile lengo la wcb kuidhihirishia dunia kwamba wao ndio wameubadilisha muziki na ndio wanautawala litakuwa limefanikiwa. kumbuka huu ni mtazamo tu sasa twende kwenye taarifa iliyo tikisa katika tasnia ya bongoflava

Akizungumza na runinga ya Wasafi, afisa mkuu mtendaji wa WCB Sallam SK alias Mendez alifichua kwamba msanii huyo ameandika rasmi kwa kundi hilo akisema anataka kujiondoa.
Sallam amesema kwamba kwa sasa moyo wa msanii huyo haupo tena na WCB na ameitisha mkutano na usimamizi wa WCB katika harakati yake ya kukubaliana na hatua hiyo.

“Harmonize kwa sasa moyo wake haupo WCB, kimkataba bado yupo. Kwa nini nasema hivo? Harmonize ameshatuma barua ya maombi ya kuvunja mkataba na yuko tayari kupitia vipengele vyote vya sheria kusitisha mkataba wake na ni kitu ambacho tumependezewa nacho. Yeye mwenyewe ameridhia na ameomba kikao na uongozi,” alisema Sallam.

Hatahivyo amesema kwamba muimbaji huyo wa wimbo ‘My Boo’ bado yupo katika mkataba wa WCB na kusisitiza kwamba ingekuwa heri iwapo Harmonise angetoka bila kuzua zahama.

“Sisi kama taasisi ya WCB tuko radhi kwa kile ambacho ataamua, hatuwezi kupinga chochote. Akiamua kufuata maelezo hayo ana baraka asilimia 100 za Wasafi na akitaka kushirikiana na Wasafi wakati wowote tuko wazi. Wajua unapoondoka kwa mazingira mazuri inasaidia uhusiano usalie pale pale,” alizungumza katika .

Kulingana na Sallam, tangazo hilo kwamba Harmonize amejiondoa rasmi WCB litatangzwa rasmi baada ya mchakato wote huo kufuatwa na kukamilishwa

“Siku ambayo atatoka kimkataba tutaangazia umma. Kwa sasa hivi ameandika barua. Nafasi yake imetoka WCB. Kufanya kazi ndani ya WCB, ndani ya moyo wake, haiko radhi tena,” aliongezea Sallam.
Sallam amesema katika tamasha la wasafi lililofanyika mjini Mwanza, kwamba Harmonise alitumia usafiri wa kibinafsi kufanya baadhi ya mambo yaliotoa tafsiri kwamba amejitenga.

”Alitufanyia mambo mengi ambayo hatukutarajia ikiwemo kumsimamisha msanii ambaye hana kibali chetu. Sisi hatupendi kuleta matabaka katika kundi letu lakini kama ilivyokuwa Harmonise aliingia kivyake, sio kwamba Diamond hawezi kufanya hivyo au Rayvany ni ile heshima kwamba WCB ina umoja na kwamba tunafuata sheria zilizopo”.

”Hatahivyo tumependezwa na hatua yake kwa sababu labda kuna vitu ameona akivifanya atafika mbali”, amesema Sallam akinukuliwa na gazeti la Mwananchi Tanzania.

Kuhusu kujitenga na wenzake Sallam amesema kwamba: Hili jambo sio sawa kulingana na maudhui ya tamasha hilo.
Maudhui ya Wasafi festival ni umoja. Msanii akiamua kuacha kuandamana na wasanii wenzake ambao wapo katika tamasha ni kwenda kinyume.

Meneja huyo amewaomba radhi wasanii wote walioshiriki tamasha la Mwanza kutokana na Harmonise kufanya jambo hilo na kwamba uongozi wa Wasafi haukuwa na taarifa.

Categories
E! News

Baada ya Flana na kofia hii hapa bidhaa nyingine kutoka kwa brand ya Fly Boy ya Wiz D

Msanii wa muziki anaetamba na wimbo wa Million Dollar Love kwa sasa, Wiz D hivi karibuni alizindua bidhaa mpya ambayo iliyopo chini ya brand yake ya Fly Boy baada ya zile za mwanzo za Flana pamoja na kofia, hivi sasa amekuja biashara mpya ya juisi.

Zenji255 ilipata bahati ya kumtembelea msanii huyo na kuweza kuzungumza na kusema kuwa, mradi huo wa juisi kwake yeye hiyo ni moja ya bidhaa ambayo kwa muda mrefu alikuwa na ndoto ya kuifanya endapo akimaliza masomo yake ya chuo.

“Nilikuwa na mpango muda mrefu na sasa nimeweza kufanya na nashukuru mungu kwa hili. Muziki sio kama ndio umenishinda, hapana, ila lazima uwe mjanja katika kutafuta na lazima uwe na vitu tofauti katika maisha ili uweze kufanikiwa” Amesema Wiz D

Categories
E! News

Chaby Six kutimiza miaka 8 kwenye muziki kiaina yake

Rapa kutoka visiwani Zanzibar, Chaby Six ambaye hivi karibuni anatarajia kufanya onyesho lake la kutimiza miaka 8 tangu uwepo wake katika saana ya muziki ambapo amelipa jina la onyesho “Usiku wa Kimewaka”

chaby six

Akizungumza na Zenji255 Chaby amesema kuwa, ni muda mrefu toka kautumikia muziki na mpaka sasa alipofikia ni sehemu nzuri kwani umemsaidia mambo mengi ndani na nje ya Zanzibar.

“Kwa sasa nashukuru mungu mpaka hapa nilipofikia, Chaby six wa sasa sio yule aliyeanza muziki kipindi kile. Imefikia wakati na mimi niwe naongea na mashabiki wangu juu ya muziki na maisha yangu, na moja wapo ndio hili naanza nalo kwa kutimiza miaka 8 ya uwepo wangu katika muziki” Amesema Chaby Six.

Katika onyesho hilo litakalofanyika tarehe 30 Juni, Chaby Six anatarajiwa kusindikizwa na wasanii kama Abramy, Catty Soul, DJ Waiz, Madawa na muigizaji Ussi Haji.

Categories
E! News

Hii hapa ni ratiba kamili ya mashindano ya BE.TALENT

Mashindano ya kutafuta vipaji mbali mbali hapa visiwani Zanzibar ya BE.TALENT ambayo yameandaliwa na lebo ya muziki ya Stone Town Records pamoja na Fumba Town Development wametoa ratiba kamili ya mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kuanza siku ya Jumamosi 23 mwezi huu saa nne asubuhi katika ukumbi wa CCM VIP club (Maisara).

Akizungumza na Zenji255 mkurugenzi wa lebo hiyo Mash Marley, amesema kuwa mashindano hayo yatakuwa na awamu mbili kwa raundi ya kwanza itafanyika CCM VIP club (Maisara) na awamu mbili kwa raundi ya pili ambayo itafanyika katika uzinduzi wa mradi wa nyumba mpya za Fumba Town Development zilizopo Fumba.

“Awamu ya kwanza itakuwa ni kutafuta washiriki ambao watatinga nusu fainali ambapo tumepanga zitakuwa siku mbili jumamosi na jumapili (23 na 24 Juni 2018) na majaji ni Baby Jay (Msanii wa muziki),  Ramadhan Journey (Mkurugenzi wa tamasha la Sauti za Busara), Salum Stika (Mwenyekiti wa chama cha waigizaji) na Mash Marley.” Amesema Mash.

Ameongezea kuwa “Nusu fainali na fainali itafanyika katika uzinduzi wa mji mpya huko Fumba ambapo raundi ya kwanza itakuwa Jumamosi 30 Juni na fainali itakuwa jumapili 1 Julai”

Fomu za usajili zinapatikana mlangoni siku ya tukio pale CCM VIP club Kuanzia saa nne asubuhi.

Categories
E! News

BE.TALENT: Hii hapa ni kwa ajili yako wewe mwenye kipaji

Lebo inayojihusisha na kusimamia wasanii wa muziki pamoja na kujishuhulisha na mambo ya kijamii, Stone Town Records imeandaa mashindano yanaoitwa BE.TALENT kwa ajili ya kutafuta vipaji katika sanaa tofauti.

Akizungumza na Zenji255 mkurugenzi wa lebo hiyo Mash Marley amesema kuwa, dhumuni la mashindano ni kuweza kuibua vipaji vipya katika sanaa tofauti ikiwemo muziki, uigizaji, uchekeshaji, dancers na nyinginezo.

“Kwa muda mrefu tulikuwa tuna malengo haya ya kufanya mashindano ila tulikuwa katika mipango ya kuweka kila kitu sawa. Zanzibar kuna vipaji vingi na tofauti, na tumeliona hili kupitia matukio mbali mbali ambayo kila siku huwa yanatokea hapa kwetu, kama vituo vingi vya habari huja Zanzibar kutafuta vipaji.” Amesema Mash.

Mash ameongezea kuwa “Kwa upande wetu sisi tukaona tusiangalie watangazaji tu, bali tuangalie pande zote ili mradi tuliwakilishe neno SANAA, Kiukweli tumejianda na kamati ipo vizuri tu hakutokuwa na upendeleo wowote”

Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza hivi karibuni. Kwa maelezo zaidi endelea kufuatilia katika mitandao yetu ya kijamii ili kuweza kujua lini, wapi na muda gani yanafanyika mashindano hayo.

Kwa wale wanaotaka kushiriki katika mashindano bonyeza hapa kwa kuijaza fomu ya ushiriki.

Categories
Awards E! News

Best Of Zenji255: Hafla ya ugawaji wa tuzo

Kwanza, tunapenda kuomba radhi kwa kuchelewesha matokeo. Data za Zenji255 zinahifadhiwa katika mitambo iliyopo Dar-es-Salaam na kwa bahati hivi juzi alhamis kulitokea hitilafu ya umeme na kuunguza baadhi ya server nakufanya tukose kutoa taarifa zetu za kila siku.

Pili, tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa wale waliohudhuria katika hafla yetu ya ugawaji wa tuzo za Best Of Zenji255. Tunayo furaha kubwa kuwajulisha kwa mwaka huu tuzo za Best Of Zenji55 zitaanza ifikapo 10 Disemba.

Katika hafla hiyo iliyofanyika siku ya Ijumaa katika chuo cha muziki kutokea Zanzibar DCMA, iliyohudhuriwa na watangazaji mbali mbali wa vipindi vya burudani hapa Zanzibar, Mkurugenzi wa chuo cha muziki cha DCMA na mwakilishi wa marehemu Mitchel Strumpf ambae alikuwa ni mvumbuzi wa blog hii, Luis.

Angalia hapo chini baadhi ya picha za hafla hiyo ya ugawaji wa tuzo za Best Of Zenji255.

This slideshow requires JavaScript.

Categories
Awards E! News

Best Of Zenji255: Hawa hapa ni washindi

Zenji255 inapenda kutoa shukrani za dhati kwa watembeleaji wote ambao walioshiriki katika upigaji wa kura juu ya wasanii wao. Shukrani pia kwa wasanii wote wa muziki hapa Zanzibar  kwa kutoa hamasa kwa mashabiki wao ili kupigiwa kura.

Shukrani pia kwa vyombo vyote habari, watangazaji wa vipindi vya burudani wote, chama cha wasanii wa muziki wa kizazi kipya (ZFU) hapa Zanzibar kwa kuweza kuipa nguvu jambo hili na kulitangaza kwa hali na mali.

Shukrani kwa wale waliofanikisha tuzo kwa njia moja ama nyingine  na kwa msaada wa njia mbali mbali. Ugawaji wa tuzo utafanyika siku Ijumaa, 2 Februari. Tunasema ahsanteni sana na huu sio mwisho bali ni mwanzo.

Tunapenda kutoa matokeo ya washindi ambao walioshinda katika tuzo za Best Of Zenji255 kwa mwaka 2017/18, ambapo kulikuwa na vipengele 8 na kila kipengele kilikuwa na raundi 2 kwa raundi ya kwanza kilikuwa na washiriki wengi lakini kwa raundi ya pili tulichukua washiriki 5 tu.

Matokeo haya ni uchaguzi wa watembeleaji pamoja na wasanii wenyewe na sio uchaguzi wa Zenji255. Zenji255 haikushiriki katika upigaji wa kura wala kupanga matokeo.

Haya hapa ni matokeo ya washindi wa tuzo za Best Of Zenji255.

STUDIO BORA: MANDEVU RECORDS

MTAYARISHAJI (PRODUCER) BORA: LUMMIE

MSANII BORA CHIPUKIZI: BOY WIZ

WIMBO BORA: FLY GIRL – WIZ D FT. ALPHA

KUNDI BORA: WATATU FLAVOR

MSANII BORA WA KIKE: HONEY ELLA

MSANII BORA WA KIUME: WIZ D

VIDEO BORA: NANI NILIMKOSEA – ISON MISTARI

Categories
E! News

Saida Karoli kurudi tena katika jukwaa la Sauti za Busara 2018

Kwa kipindi kirefu tokea mwaka 2005 mwanamuziki Saida Karoli alishiriki katika Tamasha la Sauti za Busara ambalo litaruka katika anga za Afrika mnamo tarehe 8 Februari, katika viwanja vya Ngome Kongwe Zanzibar.

saida karoli

Mwanamuziki huyo amesema kuwa ni muda mrefu hajafanya maonyesho yake katika visiwa vya Zanzibar kutokana na kuamua kupumzika kimuziki na kuangalia hali ya hewa inaendaje katika soko la muziki hapa Tanzania.

“Ni miaka 15 sasa tokea nifanye Sauti za Busara nifanye onyesho langu la mwisho katika tamasha hilo na mwaka huu narudi tena. Nikiwa na mirindimo yangu ya  zamani ni mipya, ikiwemo chambua kama karanga ambayo ilinipa jina kubwa la kuwa mwanamuziki bora wa nyimbo za asili” Amesema Saida Karoli.

Tamasha la Sauti za Busara linatarajiwa kuanza mwezi wa Februari 8 – 11, ambapo watakuwepo wasanii kutoka nchi mbali mbali za Afrika.

Categories
E! News

Picha: Hafla ya ugawaji wa mirabaha kwa wabunifu na wasanii Zanzibar

Jumuiya nya hakimiliki Zanzibar COSOZA jana Disemba 16, iliwatunuku mirabaha kwa baadhi ya wabunifu na wasanii wa tasnia mbali mbali hapa visiwani Zanzibar kwa muda wa mwaka mzima wa 2017.

Katika hafla hiyo iliyoandaliwa na mkuu wa mkoa wa mjini magharibi, Mhe Ayoub Mohammed  Mahmoud ambapo mgeni rasmi wa hafla alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria Utumushi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman.

Wabunifu na wasanii kutoka vikundi mbali mbali kutokea visiwani Zanzibar waliweza kupata mirabaha ya kazi zao pamoja na uwepo wao katika tasnia hiyo. Mhe. Ayoub alisema kuwa COSOZA itaendelea kusimamia kazi za wabunifu na wasanii ili kuona kuwa kuna maslahi, nguvu na jasho lao halipotei bure kutokana na ulaghai unaoendelea kufanywa na watu wanaozipora kazi zao.

Angalia picha za hafla hiyo iliyofanyika Baraza la Wawakilishi la zamani maeneo ya Kikwajuni, Zanzibar.

This slideshow requires JavaScript.

Categories
E! News

Best Of Zenji255: Mpigie kura msanii na mtayarishaji wako bora kwa mwaka 2017

Kwa muda wa mwaka mzima wa 2017 wasanii na watayarishaji wa muziki wengi hapa Zanzibar wameachia nyimbo nyingi na tofauti na kwa asilimia zilikuwa zikiombwa katika vituo mbali mbali vya redio na TV.

zenji255

Zenji255 kuheshimu uwepo wao katika tasnia hii ya muziki hapa Zanzibar imeamua kuweka mashindano ambayo utakayoweza wewe ukiwa kama shabiki wa wasanii hao kuwapigia kura kupitia wimbo bora, video bora, msanii bora wa kiume na wa kike, mtayarishaji bora, studio bora na mengineyo.

Kaa tayari kwa kuweza kumchagua msanii, wimbo, video, mtayarishaji na studio uliyokuwa unampenda katika kazi zake anazofanya.

Categories
E! News

Picha: Sharo Music aonekana ‘location’ akishoot video yake mpya

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Zanzibar, Sharo Music hivi karibuni alionekana ‘location’ akiwa make up artist wake akiwa katika matayarisho ya kujiandaa na kushoot video yake mpya ambayo anatarajia kuwa ndio video yake ya kufunga na kufungua mwaka.

Akizungumza na Zenji255 Shari Music amesema kuwa, anatarajia kuuanza mwaka kivingine kwani tayari maandalizi yote yapo tayari kwa ajili kuwapa raha mashabiki wake.

“Kwa sasa siwezi sema wimbo unaitwaje na umetayarishwa wapi ila ninachoweza sema ni kuwa director wa video yangu mpya ni Dully Panther ambaye ni kutoka hapa hapa Zanzibar. Na mashabiki wangu nawaomba waupokee ujio wa wimbo mpya mwishoni au mwanzoni mwa mwaka.” Amesema Sharo music.

Angalia picha za Sharo Music akiwa katika maandalizi ya kushoot video yake.

This slideshow requires JavaScript.

Categories
E! News

Zantel Yadhamini Tamasha la Wanachuo la ‘Chem Chem Bonfire ‘ Jijini Dar es Salaam.

Kampuni ya simu nchini Tanzania ya ZANTEL ilijiingiza katika burudani na kudhamini tamasha la wanachuo lililopewa jina la Chem Chem Bonfire, ambalo lilifanyika katika ukumbi New Msasani Club jijini Dar es Salaam.

Zantel

Katika show hiyo wasanii kama Juma Nature, Rich One, Young Killer na Dullah Makabila walitoa burudani kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dar es salaam lililodhaminiwa na Zantel.

Angalia baadhi ya picha ya tamasha hilo.

Juma Nature akiwapagawisha Wanafunzi kutoka Vyuo vikuu vya jiji la Dar es Salaam
Young Killer akiimba pamoja na Wanafunzi wa Vyuo vikuu vya jiji la Dar es Salaam
Msanii wa Muziki wa Singeli, Abdallah Makabila a.k.a Dullah Makabila akitumbuiza jukwaani wakati wa Tamasha la Wanachuo lijulikanalo kama ‘Zantel Chem Chem Bonfire’ lililofanyika katika ukumbi wa New Msasani Club hivi karibuni
Categories
E! News

Video: AT ashinda tuzo 2 za MAM Awards nchini Marekani

Msanii wa muziki wa miondoko ya miduara Ally Tall a.k.a AT, mnamo Jumapili Novemba 12 ameshinda tuzo 2 za Music and Movies Awards (MAM Awards) zilizofanyika katika ukumbi wa Old Greenbelt Movie Theatre nchini Marekani.

Tuzo

Akizungumza kwa njia ya simu na Zenji255 AT amesema kuwa, katika tuzo hizo walikuwa wasanii wengi waliogombania katika vipengele viwili, vikiwemo vya video bora ya muziki na msanii bora wa kimataifa.

“Kwanza napenda kumshukuru mungu, pili napenda kuwashukuru wasanii, ndugu, jamaa na marafiki zangu na watanzania wote kwa ‘sapoti’ waliyoonyesha kwangu. Kwani bila ya wao nisingeshinda hizi tuzo 2, Ushindi umerudi nyumbani” Amesema AT

AT katika tuzo hizo aliingia katika vipengele viwili vya Video bora ya muziki “Silifeel” na Msanii bora wa kimataifa.

Angalia hapo chini video fupi akiwa anatanganzwa ushindi.

 

Categories
E! News

Stone Town Records kuandaa na warsha kwa ajili ya watayarishaji wa muziki Zanzibar, Novemba 9

Lebo ya muziki ya Stone Town Records iliyopo maeneo ya Mji Mkongwe imeandaa warsha kwa watayarishaji wa muziki visiwani Zanzibar ambayo itakuwa ikifundisha mambo mbali mbali ikiwemo jinsi ya kutayarisha na kutengeneza muziki (Mixing and Mastering).

stone town recordsMmoja wa waandaji na mkurugenzi wa mipango katika lebo hiyo, Mash Marley amesema kuwa madhumuni ya warsha hiyo ni kuweza kusaidia watayarishaji chipukizi na wakongwe ambao wapo katika soko la muziki hapa Zanzibar.

“Kuna methali inasema, Elimu haina mwisho. Na lengo letu ni kuifikisha hii elimu kwa watayarishaji wetu ambao wanafanya kazi hapa kwetu. Tunataka muziki wetu uwe mzuri na wenye ubora wa hali ya juu, Zanzibar ina vipaji vizuri katika kutayarisha muziki tatizo elimu kama hizi zinakuwa ngumu kupatikana hapa kwetu” Amesema Mash Marley.

Warsha inatarajiwa kuanza siku ya Alhamis Novemba 9 itakayoanza saa nane mchana mpaka saa kumi na moja jioni, katika ukumbi wa studio ya muziki na filamu iliyopo Rahaleo, ambapo mkufunzi wa warsha hiyo atakuwa DJ Contours kutoka Ujerumani.