Zimamoto wafungwa na kipanga 1-0

0

Timu ya Zimamoto Novemba 16 walipoteza mchezo wao baada ya kufungwa na timu ya Kipanga kwa kichapo cha goli 1-0 katika uwanja wa Amani, Zanzibar.

Timu ya Zimamoto
Timu ya Zimamoto

Goli la Kipanga lililofungwa na mchezaji Is-haka Said na kuifanya timu ya Zimamoto ambayo inaoongoza ligi kuu ya Zanzibar kupoteza pointi 3.

Kwa upande mwingine timu ya Malindi iliifunga timu ya Kijichi goli 2-1 katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa Amani.

Huku timu ya Taifa ya Jang’ombe wameendelea na ushindi baada ya kuifunga timu ya Kimbunga goli 2-1 ambapo goli lao la ushindi lilipatikana kwa njia ya penalti dakika ya 90.