Zenji255 Awards 2018/19

0

Awamu ya pili ya tuzo za Zenji255 kwa mwaka 2018/19 kurudi tena  mwaka huu ambazo zinatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Katika tuzo hizo zitakuwa zinawatunuku wasanii wa muziki wa kizazi kipya ambao wanaofanya kazi zao katika visiwa vya Unguja na Pemba ikiwa ni mara pili kwa mwaka 2019 kufanyika ambapo mwaka 2018 zilifanyika tuzo na kuweza kupata washindi, bonyeza hapa kuona vipengele na washindi wa 2018.

Tuzo za Zenji255 huwa zinafanyika kila mwaka kuanzia mwezi Disemba hadi Februari ambapo huwa zinafanyika kwa awamu mbili ikiwemo raundi za mtoano. Ambapo raundi ya kwanza huchukua washiriki wote walioleta nyimbo/video katika blog ya Zenji255.com na ambapo washindi 5 watakaopita raundi ya kwanza huenda fainal na kumtafuta mshindi 1.

Kwa mwaka 2019 vipengele vitakavyokuwemo kwa awamu hii ni

  1. Video Bora
  2. Wimbo Bora
  3. Msanii Bora wa Kiume
  4. Msanii Bora wa Kike
  5. Studio Bora
  6. Mtayarishaji Bora
  7. Kundi Bora
  8. Mtunzi Bora
  9. Wimbo bora wa Kushirikiana
  10. Chipukizi Bora