Z.F.U kupambana na CCM Ofisi Kuu Ijumaa hii uwanja wa Amani

0

Chama cha wasanii cha muziki wa kizazi kipya Zanzibar (Z.F.U) Ijumaa hii (Feb.3) watacheza mechi ya kiurafiki na CCM Ofisi Kuu ya mkoa iliyopo Amani ambapo mechi hiyo itachezwa katika uwanja wa Amani.

Z.F.U

Akizungumza na Zenji255 Kiongozi msaidizi wa timu ya wasanii wa muziki, Issa Chiwile amesema matayarisho ya mechi yote yapo tayari na kwa hivi sasa wapo katika maandalizi ya kufanya mazoezi.

“Timu ya wasanii bado inaendelea na mazoezi, tunafanya katika viwanja vya Maisara kila siku kuanzia saa 10 jioni. Tunaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kwani hii ni moja kati ya burudani ukiachilia muziki lazima siku moja moja uweke sawa afya yako kwa mazoezi” Amesema Chiwile.