Wrong Turn kurudi tena ama?

0

Miezi kadhaa iliyopita kundi la Wrong Turn ambalo lilikuwa likiundwa na wasanii wawili Ison Mistari na Chaby Six lilivunjika baada ya kutoelewana vizuri kati ya wawili hao.

Lakini Oktoba 17 katika hali ya kuzangasha Chaby Six aliwashangaza mashabiki wake kupitia akaunti yake ya Facebook Chaby Six alisema kuwa anataka kuwajua mashabiki ambao wako tayari kuipokea nyimbo ya wrong turn ambayo anatarajia kuiachia Alhamis Oktoba 20.

Haijajulikana mpaka sasa kama maneno hayo aliyoyasema Chaby Six kama ni ya kweli kiupande wake.