‘Wosia wangu kwa Baraza la Sanaa Zanzibar’ – Khamis HK

0

Mwanaharakati na meneja anaesimamia wasanii wa muziki wa Zenji Fleva, Khamis HK a.k.a Kaka Meneja, kupitia ukurasa wake Instagram ameamua kutoa wosia wake kwa Baraza la Sanaa la Znazibar. Usome Hapa:

Kwa Baraza la Sanaa la Zanzibar,

Kama Hatutarekebisha hizi Sheria na Kuzisimamia ipasavyo, itafika Mahali Wasanii (Music na Filamu) Watapotea na Hatutakua na wakumlaumu zaid ya sisi wenyewe, ”Kwa sababu” Kwa hali inavyo kwenda sasa hivi, itafika Mahali Wasanii wetu Watakutana Na Msongo wa Mawazo mkubwa kwenye maisha yao, Kwa sababu Kadri wanavyo kua kiumri na miaka..

Wanazidi pia kukabiliana na Majukum zaid ya Kimaisha, na ikafika mahali Wamekua Maarufu saana na Wakashindwa ku afford Kujikim na Maisha yao na familia zao, licha ya wanavyo jitahidi Kujituma Sasa, Hasa ukizingatia Familia Zetu nyingi ni Tegemezi, Wakishindwa kufaidika apo ni Lazima Watapoteza Muelekeo, Nakujikuta Wanaingia kwenye Majanga Mbali mbali Yasio faa kwa Msongo wa Mawazo..

TUJITAHIDINI MAPEMA,KWA SOTE KUTENGENEZA MAZINGIRA YA SANAA KUA AJIRA YENYE KUTEGEMEWA KABLA HAYAJATOKEA HAYA; NI JUKUMU LETU SOTE lakini (BARAZA LA SANAA NDIO WALEZI WA WASANII WANAPASWA KUFANYA JAMBO LA HARAKA MNO). By Khamis Hk (KakaMeneja)🎤🎻🎤