Categories
E! News

Wiz D azungumzia kupita katika 5 bora ya Kali za Zenji255

Msanii Wiz D amewashukuru mashabiki wake kwa kumpigia kura baada ya kupita katika 5 bora ya kali za Zenji255 katika vipengele vinne, msanii bora, wimbo bora, chipukizi bora na video bora.

wiz d

Akiongea na Zenji255 amesema kuwa ndani ya mwaka 2016 umekuwa na mafanikio makubwa kwani toka aachie wimbo wake wa ‘Drop It’ umempatia nafasi kubwa kuonekana katika muziki wa Zanzibar na kumfanya hadi kuanzisha bidhaa zake za flana, kofia zenye nembo yake ya FLY BOY.

“Kwanza, Nashukuru sana kwa mashibiki wetu kwa nguvu kubwa waliyoitoa mpaka kunifanya mtu wao kuingia mara nne katika 5 bora ya kali za Zenji255. Hii ni kuonyesha kwamba watu wa Zanzibar bado wanahitaji mambo kama haya yawepo kwa wasanii wao. Kwani kwa miaka mingi Zanzibar hayajafanyika mambo kama haya ya kuleta ushindani baina ya wasanii na wasanii.” Amesema Wiz D.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.