Wewe ni msanii au mwanamuziki na unataka muziki wako ukue kimataifa?

0

Je unahisi sanaa yako bado inahitaji kukua zaidi ifike ngazi za kimataifa? Hii ni fursa kwa wasanii na wanamuziki kutoka Zanzibar katika kujifunza mambo mbali mbali yanayohusiana na kujitangaza kupitia sanaa husika unayofanya.

kimataifa

Warsha hiyo itaendeshwa na Jude Clark ambaye ni mwanasayansi wa tabia na mshauri katika mambo ya dijitali, ameshafanya kazi katika mambo mbalimbali ya teknolojia kwa miaka mingi nchini Uingereza, programu za mafunzo ya kufundisha na kusoma kielektroniki, alishafanya kazi kwa ajili ya BBC, RAF, Serikali ya Uingereza na wengineo zaidi.

Warsha hii itakuwa inafundisha kuhusiana na:

  • Kufahamu wewe ni nani na sanaa yako ni ipi
  • Kutengeneza mfumo mzuri wa kazi zako kidijitali – mfano utumiaji wa mitandao ya kijamii na muonekano wake unatakiwa uwe vipi
  • Jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii kujitangaza na kuongeza mashabiki
  • Misingi ya jinsi gani ya kuutangaza muziki wako

Warsha hiyo itafanyika Jambiani tarehe 9 mwezi wa 12 katika hoteli ya Red Monkey Lodge. Chai, Chakula cha mchana na vile vile usafiri wa kwenda na kurudi Stone Town kwa siku zote zitakazofanyika warsha hiyo vinapatikana.

Kama unahitaji kushiriki katika warsha hii tuma email kwa: mark@redmonkeylodge.com

Vile vile unatakiwa kuandika barua ambayo inayosema kitu kilichokuvutia kushiriki warsha hii, jieleze vizuri kuhusiana na wewe mwenyewe, kazi yako ya sanaa na nini unatarajia katika sanaa yako.

KWA MAELEZO TEMBELEA KATIKA WEBSITE YA JUDE CLARK: http://www.judeclark.co.uk