The Weeknd auza albamu yake ‘Starboy’ laki 3.5 – 4 ndani ya wiki moja

0

Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa msanii kutoka nchini Marekani , The Weeknd baada ya kuiachia albamu yake mpya ya ‘Starboy’ na kufanikiwa kuiuza albamu hiyo ya laki 350,000 mpaka 400,000 ndani ya wiki moja, na kwa dalili hizo huenda msanii huyo akakamata namba moja.

The weeknd

Katika albamu hiyo amewashirikisha wasanii kama Kendrick Lamar, Future, na Lana Del Ray na kutokana na mauzo hayo katika wiki ya kwanza yanaweza yakamfanya msanii The Weeknd kushika namba katika chati 200 za BillBoard.

Albamu yake iliyopita Beauty Behind the Madness, iliyotoka mwaka 2005 pia ilimfurahisha kwa mauzo yake japokuwa kuna tofauti na sasa kwa kuuza kopi 326,000.

Ifikapo February 2017 amepanga ataanza ziara yake za show katika nchi mbali mbali ikiwemo katika mabara ya ulaya, Amerika ya Mashariki na kwingineko.