Mashabiki wakae tayari kwa ‘Shikilia Tour’ – Sultan King

0
sultan king

Mfalme ameshasema na ahadi ni deni. Ukizungumzia wasanii wanao fanya vizuri ndani na nje ya zanzibar huwezi kukosa kulitaja jina la Sultan King anaetamba na wimbo wa Shikilia na kwa sasa Sultan King yupo katika maandalizi ya kufanya tour yake ambayo ameipa jina la Shikilia. “kuna kitu kikubwa sana nataka kukifanya siwezi kusema tarehe au ukumbi lakini naomba watu wakae tayari mwezi wa tano nitaanza kuizunguka mikoa kufanya tour yangu ya shikilia tour” alisema Sultan. Siku zote kwenye tour zozote za wasanii wanazozifanya muda mwingine huwa wanasindikizwa na wasanii wenzao na Sultan kwake yeye hakuweza kutoa jibu kwa sababu bado mapema kulizungumzia hilo. Kuhusiana na kwenda kufanya show nje ya tanzania Sultan amesema suala hilo ameuachia uongozi wake ufuatilie kwajili ya kutangaza mziki wake ndani na nje ya nchi.

Uliiona Video ya wimbo wa Shikilia kutoka kwa Sultan King