Watafutaji waelezea mipango inayofuata baada ya ‘Changamoto’ kuachiwa

0

Kundi la muziki la ‘Watafutaji’ linaloundwa na marapa wawili Buyubaya Mtabiri na Huza B, wamezungumza kuhusiana na mipango yao inayofuata baada ya wimbo wao mpya unaoitwa ‘Changamoto’ siku kadhaa zilizopita.

watafutaji

Akiongea na Zenji255 mmoja wa marapa wa kundi hilo, Huza B amesema kuwa tayari washatengenezea wimbo mwingine na upo katika maandalizi ya mwishoni ila hawapo tayari kuuachia kwani ni mapema sana.

“Tulichojipanga kukifanya kwa sasa tunaanda video ya Changamoto wakati tukiwa tunaendelea na Media tour kwani bado hatujaupeleka wimbo wetu baadhi ya mikoa hapa Tanzania hasa hasa Dar es Salaam. Na mipango kede kede ambayo ni ‘suprise’ kwa mashibiki wetu ipo njiani inakuja na tukijaaliwa tutawajulisha ikiwa tayari” Amesema Huzza B.