Wasanii Zanzibar tunaweza kufanya kazi pamoja – Mubacriss

0

Msanii Mubacriss amesema ‘show’ aliyofanya yeye na wasanii wenzake wiki iliyopita imeonyesha njia na uwezekano wa wasanii wa Zanzibar kufanya kazi pamoja.

mubacriss

Katika show hiyo mbali ya Mubacriss, wengine waliopanda jukwaani kama Rico Single, Man tuzzo, Buyu baya Mtabiri, Maco G na wasanii wengine wachanga. Mubacriss anasema hali hiyo iliongeza hamasa ya kila msanii na washabiki wake jambo ambalo anaamini litaongeza hamasa ya muziki na kuongeza ubora wa kazi.

“Ukifanya shoo na wasanii mnaopishana uwezo na uzoefu inabidi ujipange na uwe makini, hii itafanya tuwe na kazi bora kila siku” anasema Mubacriss.

Msanii huyo anaetamba na wimbo wa ‘Mapenzi mkoleni’ anasema yupo katika maandalizi ya kurekodi video ya wimbo wake ‘Haufanani’.

Aliongezea Mubacriss “Wimbo huo utarekodiwa Novemba mwaka huu baada ya kukamilika hatua zote za maandalizi”

Source: Jambo Leo