‘Wasanii wachanga lazima wawaheshimu wakongwe’ – I.T

0

Msanii wa Kizazi kipya kutoka Zanzibar Iddi Thabit ‘I.T’ amelilalamikia tatizo la wasanii wachanga ambao ndio wanaanza katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya ni lazima waheshimu wasanii wakongwe.

iddi thabit

Akizungumza na Zenji255 I.T amesema kuwa “huwa ninapata heshima kutoka kwa watangazaji wa radio, mashabiki pia wananipa heshima kama lagendary lakini wasanii wanzangu kidogo bado ila naamini ipo siku wataelewa.”

Msanii huyo ambaye hivi juzi ameachia wimbo wake mpya wa ‘Ushanivuruga’ alisema kuhusiana na video ya wimbo huo yupo kwenye mipango ya kutengeneza.