Wasanii wa Zenji & Bongo Fleva 30, Wanamitindo 10 katika jukwaa moja la Zanzibar Swahili Festival

0

Tamasha la awamu ya kwanza la Zanzibar Swahili Festival limeorodhesa list ya wasanii wa muziki na wanamitindo ambao watakaotumbuiza na kuonyesha mavazi yao katika tamasha hilo litakalofanyika April 15 na 16 katika ukumbi wa Ngome Kongwe Zanzibar.

swahili festival

Akiongea na Zenji255 muanzilishi wa tamasha hilo Sebastian Ireri, amesema kuwa tayari wameshamaliza makubaliano yote na wasanii wa Zanzibar na Bongo pamoja na wanamitindo kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania ambapo kutakuwa na maonyesho ya mavazi ya miaka kuanzia 1950 – 2000.

“Zanzibar Swahili Festival ni moja ya tamasha la kipekee ambalo lenye sura ya utamaduni wa watu wa Zanzibar katika nyanja zote na litakuwa linaendeshwa kwa kila baada ya kila miezi minne katika muonekano tofauti ili kuendeleza utamaduni wa Muziki, Sanaa na Mavazi: Michezo na burudani vile vile Chakula na maonyesho ya Biashara” Amesema Sebastian.

Wasanii wa muziki watakaokuwepo katika tamasha hilo ni: Cholo Ganun, Kimanumanu Kidumbaki, Juma Nature, Rico Single, Smile, Mr. Blue, M 2the P, Ney wa Mitego, Abramy, Nassir Vanillah, Jay Moe, Baba Rhino, Faay Baby, Baby J, T.I.D, Pozi Adim, Mirror na wengine wengi.

Kwa upande wa wanamitindo ni: Waiz, Agusta Masaki, Agnes Nyahonda, Makeke International, Mama Asiya Idarous, Sams Zubedaya, Kulwa Mkwandule, Adam Hassan, Dula Taylor, Mamy Dida na Washarudi.