‘Wasanii wa Zanzibar wanapenda vitu vya bei rahisi’ – Mantuzzo

0

Msanii Mantuzzo asema asilimia nyingi ya wasanii wa Zanzibar huwa wanapenda vitu vya bure kuanzia muziki wao mpaka ufanyaji wao wa kazi.

mantuzzo

Akizungumza na Zenji255 amesema kuwa wasanii hawapendi kujituma katika muziki wao na ndio mara nyingi hulalamika kwamba muziki wao haulipi wala haufiki kokote.

“Msanii akiingia studio anataka producer amfanyie bure kazi yake, na hata kama akilipa fedha ila sio kile kiwango kinachotakiwa. Kwa mimi hilo siwezi nikaamini kwamba muziki Zanzibar haulipi ila kama tukijituma tunaweza ila tupunguze kupenda vya bure” Amesema Mantuzzo.