‘Wasanii wa Zanzibar wafanye muziki ambao ni chimbuko kutoka Zanzibar’ – Rama B

0

Mtangazaji na mkongwe wa katika tasnia ya muziki wa Hip Hop Zanzibar Rama B amefunguka na kusema kuwa wasanii wengi kutoka Zanzibar bado hawajajitambua ni aina gani ya muziki wanafanya.

ramaAkizungumza katika kipindi cha michezo cha Swahiba FM alisema kuwa wasanii wa Zanzibar wana vitu vingi wanavikosa Rama anasema alifanya wimbo wenye mahadhi ya chakacha na kibuki na mtu akiisikiliza moja kwa moja atasema wimbo huu una mahadhi ya asili ya pwani.

“Unafikiri kwanini Offside walitoka na kufahamika kwa haraka Tanzania? Offside walikuwa wanaimba miduara na kuna vitu walikuwa wanaviongezea ambavyo vina mahadhi ya nyumbani kwao kuanzia vyombo vya muziki mpaka uimbaji.” Alisema Rama B

Rama B Aliongeza kuwa “Samaki ndio wimbo uliowatambulisha Offside na aliposikilizishwa mmoja kati ya watu wanaosimamia muziki Tanzania aliuliza ladha hii inatoka wapi. Alipojibiwa Zanzibar aliipenda sana na kusema nyinyi mmetokea Zanzibar, basi imbeni ladha za kutokea Zanzibar, lazima tupende vya kwetu.”