Wasanii wa kizazi kipya, Z.F.U kupambana na timu ya benki ya PBZ katika mechi ya hisani siku ya Mei mosi

0
wafanyakazi

Siku ya tarehe 1 mwezi wa 5 huwa ni siku ya wafanyakazi duniani, na siku hiyo kila nchi huwa inaadhimisha kwa shughuli mbalimbali. Chama cha wasanii wa muziki wa kizazi kipya Zanzibar (Z.F.U), watashuka dimbani katika uwanja wa Amani, Zanzibar kupambana na wafanyakazi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) ambapo mechi hiyo itachezwa saa 9 alasiri.

Mechi hiyo itakuwa ni ya hisani kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia waathirika wa mafuriko ya mvua na wahanga wa kipindupindu. Wasanii ambao watakaosindikiza katika mechi hiyo ni Pozi Adim, Abramy, kundi la kucheza le Benefit 7 na Jakaya.

Mgeni rasmi katika mechi hiyo atakuwa Waziri wa habari, Utamaduni na Michezo Mhe. Rashid Ali Juma na mlezi wa chama cha wasanii Mama Asha Balozi.

Kumbuka mechi ni ya hisani na kiingilio ni bure ila unachotakiwa ni kubeba japo kiasi cha pesa kwa ajili ya kuchangia ndugu zetu waliothirika na majanga ya mvua na maradhi ya kipindupindu.