Wasanii wa kike Zanzibar wajitokeze tu wasikate tamaa – Baby J

0

Mwanadada anayefanya muziki wa Bongo Fleva akiwakilisha visiwa vya Zanzibar Baby J amesema sababu za wasanii wa kike kutoka visiwani Zanzibar kushindwa kufanya vizuri katika mziki wa Bongo Fleva ni uoga.

baby jBaby J amesema kwanza kujiamini ndio kitu muhimu katika kila kazi. “Unajua Zanzibar kuna vipaji vingi vipo kama mimi nimeweza nina imani na wao pia wanaweza. Tatizo ambalo naona hasa kwa wasanii wa kike wa huku ni kutokujiamini. Unajua kila kazi inahitaji kujiamini na tatizo kubwa ambalo lipo karibu kila sehemu wasanii wa kike huwa hatupendani na hatuna ushirikiano sasa,” amesema.

“Kwa huku kwetu unajua hiki ni kisiwa kwahiyo unakuta pia ushirikiano unakuwa mdogo mtu kama mimi unajua napenda pia kukosolewa na pia kushauriwa. Hiyo hasa ndio siri ambayo hadi leo ukiuliza msanii wa kike wa Bongo Fleva anayetokea Zanzibar utasikia Baby J. Inabidi wasikate tamaa na wakubali pia kukosolewa, hizo changamoto zingine zipo kila sehemu wajitokeze tu pasipo kukata tamaa,” amesisitiza.

Chanzo: Bongo5