Vijana waliokuwa na mzuka wa ‘Muziki’ ya Darassa kupanda kizimbani leo

0

Vijana wanne waliokamatwa na jeshi la Polisi Mkoani Singida kwa tuhuma za kukiuka sheria za barabarani, watafikishwa mahakamani Ijumaa ya leo Disemba 9.

darassa

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, SSP Mayalla Towo amesema kuwa vijana hao walitafutwa na kukamatwa baada ya kusambaza video iliyowaonesha wakicheza muziki wakati gari ikiwa katika mwendo bila kujali kama walikuwa wakihatarisha maisha yao na ya watu wengine.

Amesema jambo la kushangaza, hata aliyekuwa dereva wa gari hilo aliachia usikani na kuanza kucheza huku gari ikitembea, na kisha mtu kijana mwingine ndani ya gari hilo akarukia usikani na kuendesha gari hiyo bila ya kuwa na leseni.

“Vijana wote wanne tumewakamata na tutawafikisha mahakamani Ijumaa hii, na huko watajibu tuhuma zinazowakabili ikiwemo kukiuka sheria za barabarani kwa na kuendesha gari bila leseni” Amesema Kamanda Towo.

Vijana hao walijirekodi wakiwa wanacheza wimbo wa ‘Muziki’ unaosumbua kwa sasa kutoka kwa msanii Darassa ambaye kwa upande wake akizungumza na EATV alisema baada ya kupata taarifa hizo alifanya mawasiliano na wahusika ili kuwaombea msamaha, lakini ikashindikana, na kuwaonya watu wengine wasirudie kufanya kitendo kama kile kwa kuwa ni hatari.

Waangalie vijana hao jinsi ilivyokuwa