Video: Ufaransa wafungua Euro 2016 kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Romania

0

June 10 2016 Ufaransa ambao ndio wenyeji wa michuano ya Euro 2016, walianza kucheza mechi ya ufunguzi dhidi ya Romania, Ufaransa wakiwa kwao walionekana kucheza kwa kujiamini na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1, huku hali ya umiliki wa mchezo wakiwa wamemiliki mpira kwa asilimia 51 na Romania 41.

euro 2016Magoli ya Ufaransa yalifungwa na Oliver Giroud dakika ya 57, goli ambalo lilidumu kwa dakika 8 tu na dakika ya 65 Romania wakasawazisha kwa mkwaju wa penati iliyopatikana baada ya Patrice Evra kucheza faulo na Bogdan Stancu kuitumia nafasi hiyo, furaha ya Ufaransa ilirejeshwa na shuti la Dimitri Payet dakika ya 89 baada ya kuingia wavuni.