Video Teaser: Rico Single atoa kionjo kifupi cha video yake mpya ‘Yani Raha’

0

Msanii Rico Single ameachia kionjo kifupi cha video ya wimbo wake mpya ‘Yani Raha’ ambayo aliyofanya wiki kadhaa zilizopita.

Akiongea na Zenji255 Rico amesema maandalizi yote yameshakamilika na hatua inayofuata ni anasubiri ruhusa kwa uongozi wake kwa ajili ya kuachia video.

“Video ninayo mikononi mwangu na tumejaribu na uongozi wangu kuangalia kama kuna marekebisho yoyote yanahitajika lakini tumegundua hakuna na ninawaahidi mashabiki wangu muda wowote kuanzia sasa tunavyoongea video itakuwa kwenye mitandao.” Amesema Rico Single