Video Teaser: Mabawa kuachia video ya ‘Machozi’ Oktoba 28

0

Msanii wa muziki Alatish Mabawa ambae hivi karibuni aliachia wimbo wake mpya wa Machozi uliotayarishwa katika studio za Akhenaton Records, hivi karibuni ametoa ahadi kuachia video ya wimbo huo Oktoba 28.

mabawa

Akiongea na Zenji255 Mabawa amesema kuwa Video ipo katika matayarisho ya mwisho ambayo imesimamiwa na Director Unlucky, na anatarajia kuachia Jumamosi ya wiki hii tarehe 28 katika vituo vyote vya TV nchini.

“Video tumefanya katika maeneo tofauti ikiwemo Nungwi katika hoteli ya ZALU ambapo mpaka kumaliza video nzima imenigharimu kama milioni 4 ambayo nililipia baadhi ya maeneo gharama za chakula pamoja na director kumlipia gharama zake za matengenezo ya video. Ila nashukuru mungu kila kitu kimeenda sawa” Amesema Mabawa.

Angalia kipande kifupi cha video hiyo.