Video: Man. City na Chelsea wayaaga michuano ya EFL

0

Manchester United walifika hatua ya robo fainali katika Kombe la EFL baada ya kuwalaza mabingwa watetezi Manchester City 1-0 kwenye debi iliyochezewa uwanja wa Old Trafford.

matagoalreuters

Juan Mata alifunga bao la pekee mechi hiyo baada ya kupata mpira kutoka kwa mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic.

Paul Pogba alikuwa amegonga mlingoti kwa kombora kali awali na kusisimua mechi hiyo kipindi cha pili.

Na Kwa upande mwingine:

West Ham wamefika hatua ya robo fainali Kombe la EFL baada ya kudhihirisha ubabe wao na kuwalaza Chelsea 2-1 kwenye mechi iliyochezewa uwanja wa London, zamani ukijulikana kama uwanja wa Olimpiki.

Mechi hiyo hata hivyo ilikumbwa na vurugu za mashabiki.

Askari wakiwatuliza mashabiki waliokuwa wakirusha viti na chupa uwanjani
Askari wakiwatuliza mashabiki waliokuwa wakirusha viti na chupa uwanjani

Chupa za plastiki na viti vilirushwa mamia ya mashabiki walipokabiliana karibu na mwisho wa mechi.

Cheikhou Kouyate alifunga bao la kichwa kabla ya muda mapumziko, naye Edimilson Fernandes akaongeza la pili dakika chache baada ya kuanza kwa kipindi cha pili.

Gary Cahill alikomboa bao moja dakika za mwisho mwisho lakini lilikuwa tu la kufutia machozi.

Timu ya West Ham watakutana na Manchester United katika mchezo unaofuata katika michuano hiyo ya EFL

Chanzo: BBC Swahili