Video: Aliyetobolewa macho alia baada ya kusikia wimbo wa Salome kwani hajawahi kuiona video yake

0

Ndugu Said Ally ambaye hivi karibuni lilimkuta janga la kutobolewa macho na Scorpion alijikuta anashindwa kuvumilia na kuanza kulia baada kuusikia wimbo Diamond ‘Salome’.

Akiwa katika kituo cha redio cha Clouds FM, Said alijikuta akimwaga chozi mbele ya Diamond kwani alikuwa akimpenda sana msanii huyo vile vile alikuwa hajawahi kuiona video ya wimbo wa Salome.

Msanii Diamond ambaye aliekuwepo kwenye kituo hicho amesema “Kufika kwangu hapa ni kumwambia Said kuwa kila jambo hupangwa na Mwenyezi Mungu huenda amekuepushia mambo mengi zaidi mbele.” Diamond ametoa msaada wa shilingi milioni 2 kwa ndugu Saidi Ally kwa ajili ya matibabu yake.

Angalia video hapo chini