Ussi Haji azungumzia kuhusu filamu yake mpya ya ‘THE DREAMS’

1
ussi

Na Mkali Nesta

Muigizaji wa filam Tanzania, Ussi Haji azungumzia kuhusiana na filam yake mpya iitwayo ‘The Dreams’ kuwa ipo tofauti na movies zote alizowahi kucheza akizungumza na Zenji255 alisema “Kutokana na mazingira halisi ya filam yenyewe nimefanya katika mazingira ya kifalme falme pia nimejaribu kuonyesha ufalme wa kijijini na wa mjini unakuaje vilevile.” Ussi Aliongezea “Nikajaribu kuonyesha baadhi ya matajiri wanaowadharau sana masikini, siku zote maishani ukiwa tajiri bila ya masikini haendi yaani wanategemeana kwahiyo hii ni filam ambayo inayofundisha watu wote wawe sawa” 

Ussi aliupata umaarufu kupitia filam mbali mbali za hapa nyumbani na Tanzania na kushiriki katika nyimbo wasanii mbali mbali Zanzibar alisema filam hiyo inatarajiwa kuzinduliwa mwezi wa 12 mwaka huu na kuwaomba mashabiki wake na kuwa na subira juu ya filamu hiyo mpya. “Filamu itaachiwa mwezi wa 12 mwaka huu na kikubwa ninachowaomba mashabiki wa filamu wawe na subra wanaweza ni mbali lakini sio mbali kutokana na michakato ilivyo na jinsi tunavyoelekea na tunachotaka kukifanya ni kitu kizuri kwahiyo imebidi tuanze mapema kutoa matangazo.” Alimalizia Ussi.