Ukiniuliza ni movie gani ya kuitazama CINEMA Katika wikiendi yako hapa Zanzibar… (+VideoTrailer: I shot Bi Kidude)

0
bi kidude

Siku ya Aprili 17 itakuwa ni siku ya kumbukumbu ya kifo cha mwimbaji maarufu, Bi Kidude, ambapo siku hiyo katika ukumbi wa Zancinema, Wazanzibari watapata fursa ya kuangalia filamu mbili mpya ‘Maisha ya Bibi Kidude’ na ‘Kifo cha Bibi Kidude’ zilizoandaliwa na mwanafilamu wa Uingereza Andy Jones.

Mmiliki wa Zancinema Mohamed Bajubeir alisema filamu hizo zitakuwa nzuri kwa kuwa zitakuwa zinakumbushia harakati za Bibi Kidude wakati wa uhai yake.

“Tunaonesha filamu kutoka sehemu zote duniani, hata kuna filamu chache sana kutoka Zanzibar, hii itakuwa ya kipekee,” alisema Bajubeir.

Kwa upande wa Tanzania Bara, filamu hizo zitaanza kuoneshwa Aprili 14 katika ukumbi wa Nafasi Art Space uliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Filamu ya ‘Maisha ya Bibi Kidude’ na ‘Kifo cha Bibi Kidude’ zimewahi kuoneshwa kwenye Tamasha la Kimataifa la filamu Zanzibar na kwenye Tama-sha la muziki la Sauti za Busara sambamba na matamasha mengi duniani kote na kujinyakulia tuzo mbalimbali.

Muandaaji wa filamu hizo, Andy Jones alitembelea Kisiwani Zanzibar kwa mara ya kwanza miaka ya 2000, na kuendelea kuja kila mwaka mpaka mwaka 2006 alipokamilisha filamu ya kwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari Alhamisi hii katika ukumbi wa habari maelezo, Jones alisema sababu ya kuamua kuonesha filamu hizi kwa lugha ya Kiswahili ni kuwafanya Watanzania wote waielewe kiurahisi.

“Bi Kidude alikuwa mwanamke wa watu. Ni jambo sahihi kabisha kusambaza filamu hii kwa Kiswahili ili iwafikie watu wengi iwezekanavyo.” alisema Jones.

Angalia Trailer ya filamu hapo chini.