Tunda Man azungumzia kuhusu ujio mwingine baada ya ‘Mama Kijacho’

0

Mkali wa wimbo wa ‘Mama Kijacho’ Tunda Man amezungumzia kuhusiana ujio wake wa wimbo utakaofuata baada ya kufanya ‘Mama Kijacho’.

tunda man

Akizungumza na Zenji255 Tunda Man anasema kuwa anatarajia novemba 11 kwani uongozi wake ndio utakaosema wimbo upi utaachiwa kwa sababu ana nyimbo zaidi ya moja na zote ni nzuri.

“Baada ya Mama Kijacho kuna wimbo nimefanya na Jaguar, Yamoto band na nyingine nimefanya mimi mwenyewe inaitwa ‘Mwanaume Suruali’ ila nasubiri uongozi wa Tunda Man kama mimi utoe majibu kwani ni mimi nilikuwa Tip Top lakini vile vile nina uongozi wangu tofauti kabisa na Tip Top” Alisema Tunda Man.