Toure asaini mkataba wa mwaka mmoja City

0

Kiungo wa Manchester City Yaya Toure (34) amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja katika miamba hiyo ya Manchester City na kuvunja matumaini ya timu mbali mbali zilizokuwa na nia ya kutaka huduma yake.

Toure  alijiunga city mwaka 2010 na amefunga magoli 81 katika michezo 299. Mwanzoni mwa msimu huu aliachwa nje ya kikosi kilichoshiriki michuano ya ligi ya mabingwa wa Ulaya na kisha meneja wake Pep Guardiola akaingia kwenye malumbano na wakala wa mchezaji huyo Dimitri Seluk kutoka na kutopatiwa namba ya uhakika katika kikosi cha City.