Timu ya JUDO Zanzibar yawaahidi wazanzibari kuubakisha ubingwa nyumbani

0

Timu ya taifa ya mchezo wa JUDO Zanzibar imetoa ahadi kwa wazanzibar na kuwahakikishia ya kuubakisha ubingwa katika mashindano ya East Africa Judo Champion
yanayotarajiwa kufanyika Zanzibar tarehe 4-5 mwenzi wa 3 katika ukumbi wa Amani.

judo

Akiongea na Zenji255 amesema mmoja wa wachezaji wa timu hiyo, Salma Omar Othman amesema kuwa amejipanga zaidi katika mashindano ya mwaka huu na amewataka wazanzibar wategemee ushindi wa mashindano hayo kwa upande wa wanaume na wanawake kwani wamejipanga kuhakikisha ushindi wanaubakisha nyumbani.

“Saivi ni mara yangu ya tano kushiriki mashindano ya East Africa na sijawahi kushindwa mara nyingi napata mshindi wa pili au watatu. Kwanza najiamini na nina mazoezi ya kutosha ambayo ndio nguzo kuu ya ushindi, na kilo zangu ziko za kutosha tafuti na mwanzo ambapo sasa niko kamili na naamini nitashinda” alisema Salma.

Mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika Machi 4-5 katika ukumbi wa Amani Judo, ambapo nchi zitazoshiriki katika mashindano hayo ya East africa Judo Champion ni wenyeji Zanzibar, Tanzania Bara Kenya, Burundi, Uganda, Rwanda na Ethopia.

Imetayarishwa na: Ali M. Khamis