Theo Combain na Auto Brazil kucheza mechi ya hisani kumchangia mchezaji mwenzao

0

Timu ya Theo Combain na timu ya Auto Brazil zitacheza mchezo maalum siku ya Jumamosi saa 10:15 za jioni  wa kumchangia matibabu mshambuliji wa KVZ ambae pia kwenye Ndondo hucheza Theo Kombain Yussuf Seif “Agger” mchezo ambao utapigwa katika uwanja wa Amani nje.

theo combain

Hayo yote yamekuja kufuatia mshambuliaji huyo Agger kulazwa katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja takribani wiki ya pili sasa ambapo anasumbuliwa na mchubuko tumboni wakati huo huo homa kali na viungo vya mwili wote vinamuuma.

Kocha wake wa Ndondo wa timu ya Theo Kombain Muhidin Ali “Theo” ameamua kuweka mchezo huo maalum kwa ajili ya kumchangia pesa mchezaji huyo ili apate kutibiwa kwa umakini.

“Tumeandaa mchezo huu maalum kwa ajili ya kumchangia mwana michezo mwenzetu Agger, sasa nawaomba wadau na marafiki wote ambao wanamsapoti Agger kufika pale na waje kumchangia chochote walichonacho kwasababu kama unavyojua matibabu siku hizi yamezidi kupanda bei hakuna dogo, mwenzetu yupo pale Hospitali Mnazi mmoja karibu ya wiki ya pili, na bado anasumbuliwa, tunawaomba mashabiki waje kwa wingi ili tumsaidie mwenzetu”. Alisema Theo.

Katika Mashindano ya Ndondo mchezaji huyo mara nyingi hucheza timu ya Theo Kombain na anaisaidia sana kutwaa makombe ambapo msimu ulopita tu aliisaidia Theo Kombain kushinda Ngo’mbe watatu katika mashindano ya Nyarugusu Cup, Coco Sports, Ndondo Cup pamoja na Kipwida Cup.

Chanzo: Zanzibar24