#TBT: Unakumbuka Kipindi mkate wa boflo ulivyokuwa dili?

0

Katika pekua pekua yangu ya kujikumbushia siku ya leo ikiwa ni Throw Back Thursday nilikutana na picha ambayo nilishangaa na kufurahi baada ya kuiona kwani inakumbusha mbali watu wengi na sio mimi tu.

boflo
Moja wapo ya Bekari ya miaka hiyooo. (Picha kutoka maktaba ya Narendra Gajjar)

Picha hii inanikumbusha miaka ilee ambayo ulikuwa ukiutaka mkate wa boflo lazima ukapange foleni bekari, tena kwa kuweka jiwe kwanza mapema kama ni alama ya foleni yako halafu ukija unalikuta limeshawekwa nyuma wakati ulikuwa wa mwanzo.

Unaweza kukaa masaa kadhaa kwenye foleni ukisubiri mkate na inapoanzwa kuuzwa mara kibiru kila mmoja anagombania. Halafu unarudi nyumbani na mkate uliotumwa hukuupata na familia inakusubiri wewe!

Acha kumbukumbu ibaki kumbukumbu!