#TBT: Rico Single – Hili Game (+Video)

0

Jina halisi la kuzaliwa anaitwa Rashid Amin Abdallah au kwa umaarufu anajulikana kama ‘Rico Single’ ni mmoja ya wasanii kiume wakongwe katika muziki wa kizazi kipya ‘Zenji & Bongo fleva’ kutoka visiwa vya Zanzibar.

rico1Rico Single kwa mara ya kwanza alianza kutambulika kwenye anga ya muziki wa bongofleva baada ya kuuachia wimbo wake uliotwa Kasimama Peke yake, ambao aliorekodi ndani ya studio za Jupite Records, na kweli wimbo huo ulikubalika kwa wapenzi na washabiki wa muziki huo ndani ya Zenj na hata bara kwa kiasi kikubwa.

Katika kazi yake muziki Rico Single alifanikiwa kutwaa tuzo mbali mbali, zikiwemo za mwanamuziki bora wa mwaka wa kiume muziki wa kipya, tuzo ya Amani iliyoandaliwa na tamasha la Sauti za Busara mwaka 2015 na nyingine nyingi.

rico2

Rico Single ambaye alizaliwa takribani miaka 28 iliyopita ndani ya viisiwa vya karafuu, alianza kujiingiza kwenye fani ya muziki tangu mnamo mwaka 2000, ambapo kipindi hiko alikuwa na kundi la Swahili Arts. Kundi hilo lilikuwa likijishuhulisha na mambo mbali mbali yakiwemo sanaa za maigizo, miziki, uchoraji na kadhalika. Na waliweza kutengeneza wimbo akiwa katika kundi hilo ulioitwa ‘Fadhila za Punda’ alioshirikiana na Hafidh. Kundi hilo kwa sasa halijulikani lilipopotelea

Katika mafanikio yake ya kimuziki Rico Single ameshashiriki katika matamasha kama ya ZIFF, Sauti za Busara na maonyesho mbali mbali ya ndani na nje ya nchi. Vile vile Rico Single amefanikiwa kufungua studio yake ‘Island records’.

Angalia Video ya wimbo wa Rico Single unaoitwa ‘HILI GAME’