#TBT Kutoka kwa Offside Trick – Bomba (+Video)

0

Ni #ThrowBackThursday ambayo kila siku ya alhamis huwa watu wengi hujikumbushia mambo mbalimbali ya zamani. Kwa upande wa muziki wa Zanzibar kulikuwa wasanii waliokuwa wanafanya vizuri na mpaka sasa wanaendelea na muziki. Offside Trick ni kundi ambalo mpaka sasa bado lipo lakini linaundwa wasanii wawili, Lil Ghetto na Hammer Q. Kwa miaka ya nyuma kundi hili lilikuwa linaundwa na wasanii wanne (Lil Ghetto, AT, Mudacrissna Ndevu 3) na lilikuwa likifanya shuhuli zake za muziki katika visiwa vya Zanzibar. Kundi hili lilipata umaarufu sana kupitia nyimbo zao kama Cheza, Mduara Uwanjani, Samaki, Miss Bomba na nyingine kibao. Kwa sasa baadhi wasanii waliokuwa wakiunda kundi hapo mwanzo kama vile Mudacriss na Ndevu3 wamepumzika kufanya muziki na AT anaendelea na kufanya muziki wake akiwa kama solo artist. Nimekuekea video ya offiside Trick waliyomshirikisha Spider inaitwa Bomba, video imetayarisha kampuni ya ATAS PRODUCTION ZANZIBAR.