#TBT: Baby J ft Taqwa – Mapenzi ya Kweli (+Video)

0
baby j

Baby J, wengi humfaham kwa jina hilo. Lakini jina kamili la kuzaliwa anaitwa Jamila Abdallah Ally – ni mmoja ya wasanii kike wakongwe katika muziki wa kizazi kipya ‘Zenji & Bongo fleva’ kutoka visiwa vya Zanzibar.

Msanii huyo mwenye urefu wa kiasi, kwa mara ya kwanza alianza kutambulika kwenye anga ya muziki wa bongofleva kwa wimbo wake uliotwa Mapenzi ya Kweli, aliorekodi ndani ya studio za G Records kwa Omar Saidi Kombo a.k.a KGT Shadeed, na kweli wimbo huo ulikubalika kwa wapenzi na washabiki wa muziki huo ndani ya Zenj na hata bara kwa kiasi kikubwa.

Katika kazi yake muziki Baby J alifanikiwa kutwaa tuzo mbali mbali, mnamo mwaka 2008 alipata tuzo ya ‘Msanii Chipukizi wa kike wa mwaka’ na ‘Msanii wa kike wa mwaka’ na mwaka 2014-15 alipata tuzo ya ‘Mwanamuziki bora wa mwaka wa kike’.

Baby J ambaye alizaliwa takribani miaka 25 iliyopita ndani ya kisiwa cha karafuu, alianza kujiingiza kwenye fani ya muziki tangu mnamo mwaka 2006, baada ya kufanikiwa kuibuka na wimbo wake wa kwanza uliojulikana kwa jina la Mapenzi ya Kweli.

Katika mafanikio yake ya kimuziki Baby J ameshashiriki katika tamasha la ZIFF na maonyesho mbali mbali ya ndani na nje ya nchi. Kwa sasa Baby J pia amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa chama cha wasanii wa muziki wa kizazi kipya Zanzibar (ZFU).

Angalia Video ya wimbo wake wa Kwanza kuachia akiwa amesmshirikisha Taqwa