#TBT: 2 Berry – Nakupenda (+Video)

0

Ni #ThrowBackThursday ambayo kila siku ya alhamis huwa watu wengi hujikumbushia mambo mbalimbali ya zamani. Kwa upande wa muziki wa Zanzibar kulikuwa wasanii waliokuwa wanafanya vizuri na mpaka sasa wanaendelea na muziki. 2 Berry ni kundi ambalo kwa sasa halipo tena lakini kwa kipindi hicho lilikuwa linaundwa wasanii wawili, Berry White na Berry Black. Kwa miaka ya nyuma kundi hili lilikuwa likifanya shuhuli zake za muziki katika visiwa vya Zanzibar. Kundi hili lilipata umaarufu sana kupitia nyimbo zao kama Nataka kuwa na wewe (wamemshirikisha Shirko), Raha ndani ya club, sina habari (wamemshirikisha Snare) na nyingine kibao. Kwa sasa baadhi wasanii hawa wawili kila mmoja anafanya kazi kivyake ikiwa Berry Black yupo katika usimamizi wa Saidi Fella (Mkubwa na Wanawe) na Berry White akiwa kama solo.  Nimekuekea video ya 2 Berry ambayo audio imefanywa katika studio za HeartBeat Records na producer Allan Mapigo ambayo kwa kipindi hicho ilikuwa chini ya marehemu CHUCHU. Na Video ilitengenezwa na kampuni ya Wananchi Video Production.