Tamasha la mitindo la hisani kufanyika Zanzibar

0

Tamasha la mitindo la Plus Size Fashion litafanyika Jumamosi hii visiwani Zanzibar kwa ajili ya kuchangia saratani ya matiti (Breast Cancer Zanzibar).

mitindo

Tamasha hilo limeandaliwa na kampuni ya Style House chini ya Mkurugenzi wake Mama Titi anayeishi nchini Uingereza na linatarajiwa kufanyika kwenye hoteli ya Grand Palace.

Mbunifu wa mavazi mkongwe nchini, Asia Idarous anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa tamasha hilo wakati huo huo akitarajiwa kuwa miongoni kati ya wabunifu wa mavazi watakaoonesha mavazi yao kwenye jukwaa hilo huku Wastara Juma na Khadija Kopa wakitarajiwa kuwepo pia.