Taifa Jang’ombe yatinga fainali baada ya kuifunga Chuoni kombe la mtoano

0

Timu ya Taifa ya Jang’ombe “Wakombozi wa Ng’ambo” imefanikiwa kuwa ndio timu ya kwanza msimu huu kutinga fainali katika Kombe la Mtoano baada ya kuifunga timu ya Chuoni bao 1-0 mchezo ulosukumwa Oktoba 10 saa 1:00 usiku katika Uwanja wa Amaan.

taifa jang'ombe

Bao pekee la Taifa limefungwa na Hassan Seif “Banda” kwa penalty dakika ya  60 kufuatia mlinda mlango wa Chuoni Mudathir Ali kumfanyia mazambi Banda katika eneo la hatari.

Taifa wataisubiri Sailors au Villa United “Mpira pesa” atakaeshinda katika mchezo wa nusu fainali ya pili ambayo mpaka sasa haijajulikana lini itachezwa kutokana na ratiba zilivyowabana timu hizo.

Black Sailors anashiriki ligi kuu ya Zanzibar na mpinzani wake Villa United anacheza ligi daraja la Pili Taifa Unguja huku Chama cha Soka Wilaya ya Mjini ambao ndio wasimamizi wa Mashindano hayo wanaitafuta siku ya kuchezwa mchezo huo siku ambayo haitoathiri pande zote kwenye ligi zao zilizowakabili lakini pambano hilo litachezwa usiku katika Uwanja wa Amaan.

“Hatujajua lini tutaipanga nusu fainali ya pili kati ya Sailors na Villa United kwasababu ratiba za ligi zao zinawabana lakini tukipata siku ambayo haitokuwa na athari kwa pande zote tutacheza tena usiku katika uwanja wa Amaan. Alisema Yahya Juma ambae ni katibu wa ZFA Wilaya ya Mjini.